Rais wa Rwanda Paul
Kagame anaoekana ni viongozi madikteta wanaotawala Africa baada ya
kutangaza kwamba atawania urais kwa
muhula wa tatu baada ya muhula wake wa sasa kumalizika 2017
.
Kiongozi huyo alitoa tangazo hilo kwenye
ujumbe wake wa mwaka mpya mnamo Ijumaa.
"Mumeniomba niongoze nchi hadi baada ya
2017. Kwa kuzingatia umuhimu wa hili kwenu, sina budi ila kukubali,” alisema Bw
Kahame kwenye ujumbe wake uliopeperushwa moja kwa moja kupitia runinga”.
Hii ni siku chache baada ya kufanyika asilimia
98 ya Wanyarwanda kuidhinisha marekebisho ya katiba ya kumruhusu Bw Kagame
kuwania tena.
Kura hiyo ilifanyika mwezi uliopita.
Mabadiliko hayo, ambayo yanamuwezesha kiongozi
huyo kutawala hadi mwaka 2034 imeshutumiwa na Marekani na mataifa mengine ya
magharibi.
Kagame alianza kuongoza Rwanda kama rais 2000
baada ya kuwa na mamlaka makuu tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari mwaka
1994.
Amesifiwa kwa kurejesha uthabiti katika taifa
hilo na kuendeleza ukuaji wa kiuchumi baada ya mauaji hayo.
Lakini wakosoaji wake wanasema yeye ni
kiongozi wa kiimla ambaye huwa hawavumilii wapinzani. Ametuhumiwa pia kwa
ukiukaji wa haki za kibinadamu, madai ambayo amekanusha.
Post a Comment