Rai hiyo ilitolewa na
Mwenyekiti wa chama hicho wilayani Bahi, Samwel Mlugu, wakati alipokuwa
akizungumza na waandhishi wa habari mjini hapa mara baada ya hafla fupi ya
kuwapatia msaada wa mabati walimu wastaafu.
Mlugu amesema kuwa anatoa wito k
wa Rais
Dk. Magufuli kuhakikisha anatumia kipindi chake cha uongozi kuwalipa walimu
madeni yao ambayo yameshindikana kulipwa katika awamu mbalimbali zilizopita.
Amesema kuwa kutokana na madeni ya walimu
kuwa ya muda mrefu yamekuwa yakiongezeka kila siku na kuwafanya walimu
kuendelea kulalamika bila kilio chao kutatuliwa na uongozi uliokuwepo
madarakani.
“Wakati huu serikali inaenda kutekeleza
utoaji wa elimu bure kwa wanafunzi wa kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha
nne tunamuomba Rais wetu Dk. Magufuli kuhakikisha madeni ya walimu yote
yanalipwa ili kuweza kuwaongezea ari ya kufanya kazi walimu ambao kwa kiasi
kikubwa walikata tamaa,” amesema Mlugu.
Aidha amesema kuwa katika wilaya yake
anayoiongoza walimu wanadai jumla ya Sh. 88,060,474 ambazo ni fedha za likizo,
uhamisho, posho ajira mpya, nauli na zile za wastaafu na zinginezo.
“Ni madeni ya muda mrefu sana ambayo
tunayapigia kelele kila siku lakini serikali haitaki kusikia, kuna wengine
wamekwenda likizo toka mwezi Juni mwaka huu lakini hadi leo hii tunamaliza
mwaka hawajalipwa fedha zao,” amesema Mlugu.
Naye mwalimu Iddi Nahato, amesema kuwa
pamoja serikali kulipa madeni hayo lakini pia itatakiwa kuboresha mishahara ya
walimu pamoja na kuwapatia motisha ili kuweza kuongeza ufanisi kazini.
Nahato amesema kuwa serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais Mgufuli inatakiwa kuwa na ubunifu kwa walimu ili kuweza
kuondoa manung’uniko ambayo yamekuwepo kila siku kwa walimu hali iliyokuwa kwa
kiasi fulani inachangia kushuka kwa elimu.
“Kuwepo na utaratibu hata wa kuwapatia
vyeti au motisha fulani walimu wanajituma na kuonyesha jitihada katika utumishi
wao ili kuamusha moyo wa kujituma zaidi lakini pia suala la madeni limalizwe
serikali ilipe walimu wote wanaoidai,” amesema Nahato.
Kwa upande wake mwalimu Lydia Ndyetabula,
amesema kuwa Rais Magufuli awatumia viongozi wake aliowachagua katika wizara ya
Elimu kuchunguza suala la madeni na kiini chake ili kuweza kuliondoa kabisa.
“Kaulimbiu ya Rais inasema hapa kazi tu
basi na sisi walimu tufanye kazi siyo kudai haki bila kutimiza wajibu wetu
lakini pia niwaombe wazazi kupitia elimu bure iliyoanzishwa na serikali
wasiendele kuwaficha watoto wao wawapeleke shule kwani elimu ni bure kwa wote
sasa,” amesema Ndyetabula
Post a Comment