Aibu imemkuta akiwa kazini amejikuta anakazi naye ni Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Masanja ni baada ya Rais John Magufuli
kutangaza makatibu wapya ambapo katibu huyo amekatwa jina akiwa akiwa ziarani
mkoani Mb
eya na Naibu Waziri, Dk Medard Kaleman.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Kaleman alimueleza Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abass Kandoro ofisini kwake kuwa, katika msafara wake
aliongozana na Masanja, lakini naibu katibu huyo alilazimika kuondoka alfajiri
ya jana kurudi Dar es Salaam baada ya Rais kutangaza safu mpya ya makatibu
wakuu na manaibu wao.
Kauli hiyo ilisababisha kicheko kwa maofisa mbalimbali wa mkoa na
wilaya, lakini Kandoro aliwasihi wasifurahie kwa vile mambo hayo yanaweza
kuwakuta wengi.
“Mambo haya yanashtua, hata mimi na mkuu wa wilaya na wengineo
tunafanya kazi huku tukijisikilizia. Kwa hiyo mheshimiwa naibu waziri tunaomba
mtuombee kwa Mungu,” alisema na kusababisha vicheko zaidi.
Katika uteuzi mpya manaibu katibu wa wizara hiyo wako wawili ambao
ni Profesa James Mdoe na Dk Paulina Pallangyo.
Akizungumzia sababu ya ziara hiyo, Dk Kaleman alisema alifika
mkoani hapa kukagua vyanzo vya maji yanayoingia Bonde la Usangu na hatimaye
kuingia kwenye mto Ruaha unaozalisha umeme wa Mtera, ili aweze kutoa maelekezo
sahihi kwa viongozi wa mkoa, wilaya na vijiji.
Alisema Bwawa la Mtera ambalo lilikuwa na uwezo wa kuzalisha
megawati 80 za umeme kwa sasa linazalisha megawati moja hadi mbili, baada ya
kukauka na kwamba, wakati umefika kwa wakazi wa mikoa ya Mbeya, Iringa na
Njombe kuondoka kwenye vyanzo vyote vya maji.
Kwa upande wake Kandoro alisema tayari ameandika barua kwenda
katika wizara hiyo kuomba kikao kitakachohusisha wizara za Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi; Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Maji pamoja na Maliasili na
Utalii ili kuweka mkakati wa kuliokoa bwawa hilo.
Naibu
waziri huyo jana alikwenda katika vijiji viwili vilivyoko kwenye milima ya
Mporoto ambako kuna vyanzo vingi vya maji.
Post a Comment