Waumini wa dini ya kislamu dhehebu ya Shia wapinga jeshi la nchi hiyohuku
maandamano hayo
yalishuhudiwa katika
miji sita mita mikuu, mji wa Kaduna ukiathirika zaidi.
Rais wa Iran, Hassan
Rouhani alimpigia sim
u mwenzake wa Nigeria Muhammadu Buhari kuhusu operesheni
hiyo ya jeshi.
Iran ni taifa la
Kishia.
Jeshi la Nigeria
linatuhumu dhehebu hilo la Kishia kwa kujaribu kumuua mkuu wa jeshi Jenerali
Tukur Buratai.
Dhehebu hilo kwa jina
Islamic Movement of Nigeria (IMN), limekanusha madai hayo.
Kwa mujibu wa vyombo
vya habari vya Iran, kwenye mawasiliano yake na Bw Buhari, Bw Rouhani aliuliza
kuhusu hatima ya Sheikh Ibraheem Zakzaky, kiongozi wa IMN aiyekamatwa baada ya
wanajeshi kuzingira nyumba yake katika mji wa Zaria.
Dhehebu la IMN
linasema mamia ya waumini wake waliuawa na wanajeshi na madhabahu ya kundi hilo
yakaharibiwa kwenye operesheni ya kijeshi.
Mtetezi wa haki za
kibinadamu Chidi Odinkalu, ameunga mkono takwimu zinazotolewa na kundi hilo na
kumtaka Rais President Buhari kuunda tume huru ya uchunguzi
“Haiwezekani.
Wanigeria wana haki ya kuishi. Jeshi linawezaje kukabili watu wanaoandamana
wakirusha mawe kwa bunduki?” Bw Odinkalu ameongeza
Kundi la IMN lina
makao makuu yake IMN na wafuasi wa dhehebu hilo waliandamana, huku vikosi vya
usalama vikishika doria.
Mwandishi wa BBC Nura
Muhammed Ringim anasema watu wengi walisalia manyumbani wakihofia usalama.
Miji ya Kano, Katsina,
Sokoto, Zamfara na Bauchi pia ilishuhudia maandamano.
Nchini Iran, kundi la
watu lilikusanyika nje ya afisi za Umoja wa Mataifa mjini Mashhad kupinga
maandamano hayo, kwa mujibu wa shirika la habari la kibinafsi la Tehran Tasnim.
Jeshi halijatoa idadi
ya watu waliofariki, lakini limekanusha madai kwamba mkewe kiongozi huyo wa IMN
Zeenat Ibrahim aliuawa.
Meja Jenerali Oyebado,
mkuu wa jeshi wa Kaduna, alisema Jumatatu kwamba mwanamke huyo anazuiliwa na
jeshi.
Hakuthibitisha wala
kukana madai ya kuuawa kwa mwana wa kiume wa Sheikh Ibraheem Zakzaky, Sayyid
Ibraheem Zakzaky.
Mwaka uliopita, wana
watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky waliuawa kwenye makabiliano kati ya jeshi na
wafuasi wa dhehebu hilo.
SOURCE BBC
Post a Comment