Watanzania wanalazimika
kuikimbia nchi yao na kuishi kwa mashaka hii inawahusu wafugaji waliovamia
maeneo ya wakulima katika kijiji cha Dihinda wilayani Mvomero mkoani Mogorogo
na kusababisha mapigano yaliyoua mkulima na ng’ombe 71, wamekimbia kijijini
hapo na kutokomea kusikojulikana.
Akizungumzia hatua
zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Wilaya ya Mvomero, Mkuu wa Wilaya
hiyo, Betty Mkwasa alisema ulinzi bado umeimarishwa eneo hilo, na kwamba
wafugaji waliovamia wamekimbia.
“Wafugaji wamekimbia na
sisi tutateketeza maboma yao, kwa sababu walivamia eneo hili la wakulima na
ng’ombe walioachwa wamepigwa mnada na fedha imeingizwa kwenye mfuko wa serikali
ya kijiji hicho,” alisema Mkwasa.
Aidha, katika msako
uliofanywa kwa ushirikiano wa Serikali ya Wilaya na Polisi silaha moja ya
askari iliyochukuliwa ilipatikana na kwamba wakulima wametolewa hofu na
kusisitizwa kuendelea na kazi zao kama kawaida.
Alifafanua kwamba hali
kwa sasa kijijini hapo ni shwari na kwamba mifugo iliyouawa kwa kukatwakatwa
mapanga yote imeshafukiwa na uongozi wa serikali ya wilaya umepanga kuingia
mkataba na viongozi wa vijiji na kata ili kudhibiti, migororo baina ya makundi
hayo.
Alisema katika kudhibiti
matukio ya mapigano au uvunjifu wa sheria na mpango wa matumizi bora ya ardhi,
Mvomero itaanza kuingia mkataba na watendaji wa vijiji na kata na iwapo
migogoro itatokea, wao ndio watawajibishwa.
Awali Desemba 12, mwaka
huu, kundi la wafugaji wa jamii ya Kibarbaig waliwavamia wakulima na kuanza
kuwashambulia kutokana na mmoja wa wafugaji ambaye mifugo yake iliharibu mazao
ya mkulima kutakiwa kulipa fidia ya Sh 200,000. Katika tukio hilo.
Post a Comment