Wafugaji nchini
Tanzania wametoa tamko la pamoja serikali kuwajibika kwa
kuhakikisha
wanakabiliana kwa haraka na tatizo hilo jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa
migogoro isiyoisha.
Amesema migogoro mingi
ya ardhi haiwaathiri tu wafugaji pekee bali inayakumba makundi mengine na
kusababisha kuwepo kwa matatizo mengine.
Alivitaja vyanzo vya
migogoro hiyo amesema kuwa ni Sheria ya utambuzi wa mifugo 2010 kuanzia
uhamiaji wa wafugaji wa asili na mifugo, Sheria ya wanyamapori 1998 inazuia
uhamiaji wa wafugaji katika maeneo ya wanyamapori ilihali maeneo mengi
yanayofaa kwa malisho yakitwaliwa kwa ajili ya uhifadhi.
Walitaja sababu
nyingine ambazo zinasababisha migogoro ni pamoja na Sheria ya hifadhi ya
mazingira ya Mwaka 2007 inaainisha kuwa ufugaji wa asili ni moja ya vyanzo vya
uharibifu wa mazingira jambo linalopotosha jamii na kusababisha migongano baina
ya wafugaji asili, Mamlaka husika na makundi mengine, licha ya kwamba ufugaji
asili ni rafiki wa mazingira.
Amesema kutokana na
kuwepo kwa migogoro ya ardhi hiyo kunapelekea watu kuuwawa huku mifugo nayo
ikiuwawa jambo ambalo linasababisha umasikini.
“Migogoro ya ardhi
imesababisha kuwepo kwa vifo vingi vya watu mifugo, majeruhi na ulemavu wa
kudumu, uharibifu wa mali na mazao mashambani, kuzorotesha shughuli za
uzalishaji mali kutokana na hofu miongoni mwa wanajamii, umasikini, visa na
chuki miongoni mwa jamii, ubakaji na vingine vya ukiukwaji wa haki za binadamu
pamoja na uharibifu wa makazi,” amesema Muro.
“Kutokana na kuwepo
kwa matukio hayo umoja huo taasisi zisizo za kiserikali tunachukua hatua hii
kulaani, vitendo vya uvunjifu wa amani ,haki za kibianadamu na za wanyama
vilivyojitokeza wilayani Mvomero na Kilosa Mkoani Morogoro Desemba 14 mwaka huu
vilivyopelekea vifo watu na mifigo.
“Kwa kauli moja
tunatoa tamko la kuitaka serikali iwajibike na kumtaka waziri ardhi kubainisha
na kuweka wazi maeneo yote ya wafugaji yaliyoodhiwa na wawekezaji wasio rasmi
na wasio rasm ili yarejeshwe kwa wafugaji.
“Serikali kwa
kushirikiana na wadau iwe mkakati wa pamoja wa kuelimisha Umma juu ya umuhimu
wa amani baina ya makundi yote katika jamii na kulinda haki ya kila mmoja,”
lilisema tamko hilo lenye mambo 8.
Kwa upande wake
mwakilishi wa Katibu mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Anociata
Njombe alikiri kuwepo kwa mgogoro wa ardhi kwa muda mrefu ambao kwa sasa
unatafutiwa suluhisho na serikali ya awamu ya tano.
“Pamoja na ukweli
kwamba ufugaji ni shughuli ya kiuchumi kwa hapa nchini bado lipo pengo la
kisera katika kukidhi malengo na mahitaji halisi ya kuboresha ufugaji wa
asili,” amesema.
Amesema ni kweli
wafugaji wanaendelea kukabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za ukosefu wa
maeneo ya malisho kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Amesema kuna
changamoto nyingine ambayo ni ukosefu wa malisho na maji, magonjwa ya mifugo na
ukosefu wa huduma za jamii katika maeneo ya wafugaji asili.
“Changamoto hizi
zimezidi kuongezwa makali na kasi ndogo ya migango ya matumizi ya ardhi na
kutenga maeneo kwa ajili ya wafugaji,” amesema Njombe.
Post a Comment