Ukweli kuhusu uzazi wa
mpango
Uzazi wa mpango ni nini?
Uzazi wa mpango ni
maamuzi ya hiari ya mtu au wenza juu ya ni wakati gani waanze kuzaa, watoto
wangapi wazae , wapishane kwa umri gani na lini waache kuzaa.
Kwa nini uzazi wa mpango
ni muhimu?
Kipindi cha Ujauzito
kinaweza kikawa ni hatari kwa mama na motto hususani kinamama wakipopata
ujauzito katika umri mdogo sana/mkubwa
, muda mfupi baada ya kujifungua au
wakizaa watoto wengi. Asilimia kumi na saba 17% ya vifo vyote vya kinamama wa
kitanzania kuanzia umri wa miaka 15-49 hutokea wakati wa ujauzito, wakati
wanajifungua ndani ya kipindi cha miezi miwili baada ya kujifungua au kutoka
kwa mimba (TDS ) . Vilevile mtoto mmoja kati ya watoto ishirini wa kitanzania
hufariki dunia kabla ya kutimiza umri mwaka moja baada ya kuzaliwa. Njia
mojawapo bora ya kuzuia vifo vya kinamama na watoto vitokanavyo na uzazi ni
kuzuia mimba zisizopangwa/zisizotarajiwa na njia nzuri ya kujikinga na hili ni
kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.
Nini hali halisi ya uzazi
wa mpango Tanzania?
Ingawa kuna ongezeko la
watu wanaotumia njia za kisasa za uzazi wa mpango lakini pia kuna ongezeko la
watoto 5.4 wanaozaliwa kwa kila mwanamke mmoja. Utafiti unaonyesha wanawake
wengi huzaa mapema ambapo asilimia ishirini na nane 28% huzaa katika umri wa
miaka 18, asilimia hamsini na tano 55% umri wa miaka 20 na asilimia themanini
na nane 88% umri wa miaka 25.
Tafiti hii inaonyesha
kuna umuhimu wa kutoa elimu juu ya uzazi wa mpango kwa vijana, kwa watu ambao
hawajaoa au kuolewa. Vilevile kuna ulazima wa kuwalenga pia wenza (wanaume).
Pia asilimia sabini 70%
ya wanawake walioolewa wanatamani kuchelewa kupata watoto au kupanga idadi ya
watoto watakaowazaa lakini ni asilimia ishirini na saba 27% ya wanawake hao
hutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango. Ambapo asilimia
tano 5% hutumia njia za
muda mrefu na njia za kudumu za uzazi wa mpango.
Uzazi wa mpango una faida
gani?
Pamoja na kumuwezesha
mama na mtoto kuwa na afya njema, uzazi wa mpango una faida nyingi kwa
wanawake, wanaume, watoto, familia na jamii kwa ujumla:
• Unamsaidia mama kurudi
katika hali yake ya zamani ambayo ilisumbuliwa na hali ya ujauzito, uchungu na
kujifungua, mama atakuwa mwenye nguvu, afya nzuri na mchangamfu. Na pia atakuwa
na muda mzuri wa kurudisha afya yake kabla ya kupata ujauzito mwingine.
• Unamuwezesha kuhudumia
familia yake vizuri na kuwa na maisha bora. Utakuwa na muda, fedha na mahitaji
muhimu kwa familia yako kama chakula, mavazi, elimu, mapenzi na huduma zote
muhimu.
• Mama anapata muda wa
kutosha wakujishughulisha na mambo mengine ya kiuchumi na kimaendeleo kwa ajili
ya familia na jamii kwa ujumla.
[5:44PM, 12/13/2015]
mimaz: • Mama na baba wanapata muda mzuri wa kujishughulisha zaidi na mambo na
mahitaji yao binafsi.
• Unasaidia kukuza uchumi
na maendeleo ya nchi.
Nani anapaswa kutumia
uzazi wa mpango?
Yoyote mwenye umri wa
kuzaa au anatarajia kufikia umri huo anapaswa kufikiria kuhusu uzazi wa mpango.
Uzazi wa mpango ni muhimu kwa:
• Wanawake na wanaume
• Watu walioa na kuolewa
au ambao hawajaoa wala kuolewa
• Watu wenye watoto au
bado hawajapata watoto.
Ni wakati gani mtu atumie
uzazi wa mpango?
Umri sahihi wa kuanza
kutumia uzazi wa mpango ni kuanzia miaka ishirini (20) na thelathini na
tano(35). Ujauzito ni hatari kwa mama na mtoto endapo mama
atajifungua chini ya umri
wa miaka ishirini (20) au zaidi ya miaka thelathini na tano (35) vilevile ni
hatari kwa mama atakaejifungua zaidi ya watoto wane au
hasipowapishanisha
watoto. Wenza wanatakiwa kusubiri angalau miaka miwili kabla ya kupata mtoto
mwingine pia wafikirie kutumia njia za kisasa za uzaziwa mpango wakati wote
ambao hawajapanga kupata mtoto.
Njia za uzazi wa mpango
ni zipi?
Kuna njia nyingi za uzazi
wa mpango ambazo zinaweza kutumiwa na mtu au wenza waweze kusubiri,
kuchelewesha, au kupunguza idadi ya watoto watakaowazaa. Zipo njia za mda
mfupi, mda mrefu na za kudumu.
• Njia za muda mfupi:
Hizi ni njia za kisasa za
uzazi wa mpango ambazo unaweza kuzibadilisha. Unaweza kupata ujauzito pindi
utakapoacha kuzitumia. Njia hizi ni nzuri kwa mama
anayetaka kupata ujauzito
baada ya miaka miwili baada ya kujifungua.
Nazo ni: -
Njia ya vichecheo
Njia hizi zina vichocheo ni
sawa na vichocheo vya kawaida vilivyomo kwenye mwili wa mwanamke.
Njia ya vidonge
Vidonge hivi hutumiwa na
wanawake kila siku.
Njia ya sindano
Mama huchoma sindano kila
baada ya miezi mitatu (3). Njia ya dharura ya vidonge vya uzazi wa mpango
Humezwa na mama ili kuzuwia kupata mimba kwa mama
aliyetenda ngono bila
kutumia kinga yeyote. Hivi vinaweza kuzuwia mimba hadi siku tano baada ya
kujamiana.
Njia za Kizuizi
Kondom za kike na kiume.
Ni muhimu kutumia ipasavyo kila unapofanya ngono. Hii ni njia ya pekee ambayo
pia inazuia maambukizi ya VVU na magonjwa ya zinaa.
[5:44PM, 12/13/2015]
mimaz: Njia za asili
Kukosa hedhi kwa
kunyonyesha mfululizo Hii ni njia ya asili ambayo inatokea kwa mwanamke
anayenyonyesha na ni ya kuaminika zaidi wakati mama huyo bado hajaanza kuona
siku zake za hedhi na ili hayo yote yatokee ni lazima mama awe anamnyonyesha
mwanae mara kwa mara usiku na mchana na Mtoto awe na umri chini ya miezi sita
(6).
Elimu ya kujua siku za
hatari uzazi
Hii inawezekana ikiwa
mama anaufahamu mzunguko wake mzima wa siku zake za hedhi na kujua ni zipi siku
za hatari za kushika mimba. Yeye na mwenza wanatakiwa kuacha kabisa kufanya
ngono siku hizo za hatari.
Kukojoa nje
Hii inafanywa na
mwanamume wakati wa tendo la ndoa ambapo humwaga shahawa zake nje ya uke.
• Njia za muda mrefu:
Hizi ni njia ambazo pia
zinaweza kurudiwa. Unaweza kupata ujauzito mara utakapoacha kuzitumia. Hizi ni
nzuri ikiwa unataka kusubiri zaidi ya miaka miwili kabla ya kupata mtoto mwingine.
Njia ya vipandikizi
Hiki ni kijiti cha
plastik anachowekewa mwanamke chini ya ngozi kwenye mkono wake kinaweza kuwa
kimoja au viwili. Hivi huzuia mwanamke asipate ujauzito kwa muda kati ya miaka
3 hadi 5 kutegemea na aina ya vipandikizi alivyotumia.
Njia ya kitanzi
Ni kifaa kidogo chenye
shaba na plastiki ambacho huwekwa kwenye mji wa mimba. Hichi hukuzuia usipate
mimba mpaka miaka kumi na mbili (12), unaweza kukitoa wakati wowote utakapoamua
au kuhitajia kupata mtoto.
• Njia ya kudumu:
Hizi ni njia huwezi
kuzirudia na ukitumia huwezi kupata mtoto tena. Na hutumiwa na watu ambao
hawataki kupata mtoto tena. Nazo ni: -
Kufunga kizazi kwa
mwanaume
Njia hii inahusisha
upasuaji mdogo ambapo mirija ya uzazi ya mwanaume ukatwa au kufungwa hivyo
kuzuia yai kusafiri na kukutana na shahawa. Mwanaume anaendelea kuwa na hamu ya
kujamiiana na kutoa mbegu lakini mbegu zake hazitaweza kutunga mimba
Kufunga kizazi kwa
mwanamke
Njia hii inahusisha
upasuaji mdogo inafanyika kwa kuziba au kukata mirija ya kizazi kuzuia yai
kukutana na mbegu. Mwanaumke ataendelea kuwa na hamu ya kujamiiana na kuona
siku zake za hedhi.
Utafahamu vipi kuwa njia
gani ya uzazi wa mpango ni sahihi kwako?
Inategemea na mtu
mwenyewe au wenza kuamua njia gani ni sahihi kwao. Tembelea kituo cha afya
kilicho karibu nawe uonane na wahudumu wa afya wataweza kukufahamisha njia
sahihi kwako. Pia unaweza kutuma
ujumbe mfupi M4RH kwenda
15014 BURE kwa maelezo zaidi.
Ni nini Madhara ya njia
za uzazi wa mpango?
Njia za kisasa za uzazi
wa mpango hazina madhara na zinafanya kazi vizuri zikitumiwa kwa ufasaha.
Yafuatazo ni madhara madogo madogo ya njia za uzazi wa mpango ambayo ni ya
kawaida na hayana madhara. Pia sio dalili ya maradhi. Mama wengine wanaweza
kuona: -
• Mabadiliko ya siku za
hedhi, Kutokwa na damu nyingi wakati wa siku za hedhi au damu kidogo au kukosa
kabisa
• Maumivu ya kichwa
• Matiti kujaa
• Mabadiliko ya uzito
• Kizunguzungu
Madhara mengi yanapungua
au kuisha ndani ya miezi michache baada ya kuanza kutumia njia za uzazi wa
mpango. Ni wanawake wachache hupata matatizo baada ya kutumia njia za uzazi wa
mpango. Ukipata matatizo yoyote nenda kituo cha Afya kilicho karibu nawe.
Vipi njia za uzazi wa
mpango unaathiri uwezo wa
kupata mtoto
Njia za kisasa za uzazi
wa mpango hazimfanyi mtu kuwa tasa. Njia kama kondom, vidonge, kitanzi na
vipandikizi unapoviacha tu mwanamke anaweza kupata ujauzito. Inawezekana
mwanamke kuchukua miezi michache kupata ujauzito kwa yule aliyetumia sindano.
Hii ni hali ya kawaida na mwanamke hana haja ya kuwa na
wasiwasi.
Kuna njia mbili za kudumu
za kufunga kizazi kwa mwanamke na kufunga kizazi kwa mwanaume ambazo hawataweza
kupata mtoto tena. Hizi ni kwa wale ambao wameamua kutopata mtoto tena katika
maisha yao. Ni vizuri ifahamike kuwa uzazi unapungua kadiri mwanamke
anapoongezeka umri. Unaweza kwenda kwenye kituo cha afya kilichopo karibu nawe
wakati wowote ikiwa una tatizo lolote, maswali au ikiwa unataka kubadilisha
njia za kisasa za uzazi wa mpango.
Post a Comment