Waziri aliemuondolea imani kwa watanzania Raisi John Pombe
magufuri anza kuthibitisha kuwa yeye ni chaguo sahihi kwa baada
ya kuanza na Shirika
la Umeme Nchini (Tanesco) limetakiwa kuandaa mpango madhubuti wa utitirishaji
maji kutoka kwenye bwawa la Nyumba ya Mungu ili kuwepo na maji ya kutosha
kuzalisha umeme kwenye vituo vya Hale na New Pangani.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo alitoa
agizo hilo wakati wa ziara yake katika mabwawa ya kuzalishia umeme ya
Hale na Pangani yaliyoko mkoani Tanga na bwawa la Nyumba ya Mungu la
mkoani Kilimanjaro.
Agizo hilo alilitoa baada ya kujionea namna ambavyo kina cha
maji kwenye mabwawa ya Hale na Pangani kimepungua kutokana na mipango hafifu ya
utiririshaji maji kutoka bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo ni chanzo kikuu
cha upelekaji maji katika mabwawa hayo yaliyoko mkoani Tanga.
Profesa Muhongo alisema wananchi wanatarajia umeme
usiokatikakatika, umeme wa kutosha na wa bei nafuu.
“Nimeamua kufanya ziara katika vyanzo vyote vya uzalishaji umeme
nchini ili baada ya hapa tuangalie jinsi tutakavyoboresha hali ya uzalishaji
umeme na wananchi wetu wapate umeme wa uhakika na wa bei nafuu,” alisema Profesa
Muhongo.
Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme wa maji wa Pangani, Mhandisi
John Skauk alisema kuwa mitambo ya Hale ilifungwa mwaka 1964 ikiwa na uwezo wa
kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati 21 ambapo kila mtambo (kati ya mitambo
miwili) katika kituo hicho una uwezo kuzalisha umeme wa kiasi cha megawati
10.5.
Aliongeza kuwa ukarabati wa kwanza wa mitambo hiyo
ulifanyika mwaka 1986 na kuwa ilipofika mwaka 2008 mtambo mmoja uliharibika na
hivyo kusababisha mtambo mmoja tu kufanya kazi hadi sasa.
Akionekana kukasirishwa na taarifa hiyo, Profesa Muhongo
alihoji ni kwanini ukarabati wa mtambo huo umechukua muda mrefu na na
kuagiza mtambo huo kufungwa haraka ili uweze kuzalisha nishati ya umeme.
Profesa Muhongo pia alisisitiza kufanyika kwa ukarabati wa mara
kwa mara wa mitambo ya uzalishaji umeme huku akielezea kuwa kuchelewa kwa
ukarabati wa mitambo hiyo ni sababu mojawapo ya matatizo ya umeme nchini.
Kwa upande wa kituo cha uzalishaji umeme cha New Pangani
ilielezwa kuwa mitambo iliyopo ina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 68 hata
hivyo kutokana na upungufu wa maji kwenye bwawa la Pangani mitambo hiyo
inazalisha megawati 17 hadi 50 kwa siku.
"Mitambo hii ya Pangani iko vizuri haina hitilafu yoyote
isipokuwa tu ni suala la kutopata maji ya kutosha kutoka kwenye chanzo kikuu
ambacho ni Nyumba ya Mungu," alisema Mhandisi Skauk.
Aidha, akizungumzia Kituo cha Nyumba ya Mungu, Mhandisi Skauk
alieleza kuwa kituo kinao uwezo wa kuzalisha jumla ya Megawati nane hata hivyo
kiasi hicho hakijafikiwa kutokana na utiririshaji mdogo wa maji hivyo kwa sasa
kinazalisha Megawati 3.7.
“Tunashindwa kutiririsha maji ya kutosha kwa sababu tukifanya
hivyo tutasababisha mafuriko kwenye baadhi ya maeneo ambapo maji hayo
yanapita,” alisema.
Akizungumzia kwa ujumla suala la uzalishaji umeme kwa kutumia
maji, Profesa Muhongo alisema kuwa changamoto ya uzalishaji umeme wa maji
nchini inatokana pia na mabwawa mengi kujengwa kwa kutumia teknolojia ya zamani
hivyo Serikali imedhamimiria kuwa na vyanzo vingi zaidi vya kuzalisha nishati
hiyo ya umeme mbali na maji.
"Lazima tuwe na vyanzo vingi, umeme upatikane,
usikatikekatike. Tunafanya tathmini ya vyanzo vyote tuone uzalishaji wake,
ziara hii ni muhimu kwani bila kufanya hivi nisingejionea kwamba kuna mtambo
haufanyi kazi tangu mwaka 2008,” alisema Muhongo.
Alisema alichokiona Kanda ya Kaskazini ni kuwa maji yapo ya
kutosha isipokuwa hakuna mipango madhubuti ya kutiririsha maji kutoka kwenye
chanzo kikuu hadi kufika kwenye mabwawa ya uzalishaji umeme ya Hale na Pangani.
"Habari ya kuwa mnawaambia wananchi kwamba huku hakuna maji
sio sahihi. Maji yapo isipokuwa hakuna mipango mizuri ya mtiririko wa maji
kutoka Nyumba ya Mungu kwenda Hale na Pangani," alisema.
Alisema vyanzo vya umeme wa maji nchini vinapaswa kuzalisha
Megawati 561 lakini umeme unaozalishwa kwa njia hiyo kwa sasa si zaidi ya
Megawati 110 ambayo ni sawa na asilimia 20.
"Hili suala la maji linatia aibu; tunataka tutathmini ndani
ya siku kumi tubaini wapi tuongeze nguvu zaidi, Tanesco inapaswa iingie gharama
ya kutengeneza miundombinu ya maji," alisema Profesa
Muhongo.
Aliliagiza Shirika hilo la Umeme kufanya kikao na Bodi ya Bonde
la Pangani ili kuandaa mpangilio mzuri wa kuruhusu maji kutoka bwawa la Nyumba
ya Mungu hadi Hale na Pangani bila kuleta uharibifu kwa kuwa wananchi pia
wanahitaji maji hayo kwa matumizi mbalimbali.
Aliagiza kikao hicho kifanyike tarehe 15 mwezi huu (Jumanne)
asubuhi na makubaliano ya kikao yapelekwe Wizara ya Nishati na Madini na wakuu
wa wilaya wa maeneo husika ili hatua zichukuliwe haraka.
Post a Comment