viongozi wa mataifa wa Umoja wa Ulaya kukutana kwa viongozi wa ulaya ni kujenga Syria moja na kulete maendeleo ambayo yamesimamishwa baada ya kupiga kwa muda mrefu
Wale
watakaohudhuria wanatarajia kujadiliana pendekezo la kutaka kuwapa watu kutoka
Syria walio katika kambi nchini Uturuki makaazi moja kwa moja.
Hata
hivyo Chanse
la wa Ujerumani Angela Merkel, aliyetoa pendekezo hilo,
anakabiliana na upinzani mkali kutoka mataifa mengine ya Ulaya.
Mkutano
wa viongozi wa Umoja wa Ulaya unaopaswa kufanywa Alhamisi unatarajiwa kumulika
tatizo la uhamiaji ambalo limegawa wanachama wa Jumuiya hiyo.
Watu
wengi wamewasili Ulaya mwaka huu, jambo ambalo limeyafanya mataifa mengine
kujenga nyua kwenye mipaka yao ili kuanza kuthibiti mienendo ya wahamiaji hao.
Wakati
huohuo mataifa mengine wanachama yameanza kupuuza mapatano ya Schengen, ambayo
yanaruhusu raia wa mataifa hayo ya ulaya kutembeleana bila vibali au mtu kupata
visa moja ya kutembelea mataifa yote wanachama wa Umoja wa Ulaya.
Pendekezo
hilo mpya litashuhudia mataifa wanachama wa Jumuiya ya Ulaya yakiwakubali
wakimbizi wa Syria wanaotoka kambi za Uturuki moja kwa moja chini ya mpango wa
kujitolea.
Inatarajiwa
kuwa mpango huo utasitisha watu kusafiri mwendo hatari kupitia bahari hadi
Ugiriki na pia wanachama wa Jumuiya hiyo kufurahia mpango huo kuliko kupokea
idadi ya watu ambayo wamelazimishiwa.
Mwezi
uliopita Uturuki na viongozi wa Ulaya walikubaliana kuwa Uturuki itawazuia
wahamiaji kuondoka nchini mwao ambapo mataifa ya Ulaya nayo yatalegeza masharti
ya kifedha na kisiasa kwa Uturuki.
Mkutano
wa viongozi wa Umoja wa Ulaya utajadiliana jinsi ya kuunda kikosi cha muungano
huo cha kushika doria fuo za mataifa hao na njia za kuthibiti mipaka yake.
Vita
dhidi ya ugaidi ni swala ambalo litamulikiwa pia katika mkutano huo kwa kuwa
imethibitishwa sasa kuwa wawili kati ya washambulizi waliohusika katika
shambulio la Paris Ufaranza walitumia njia inayofuatwa na wahamiaji kufika
Ufaransa.
Wahamiaji
wengi wanatoroka manyumbani kwao kutokana na ghasia katika mataifa kama vile
Syria, Iraq na Afghanistan, wakitafa kufika Ulaya.
Post a Comment