Wanasema visa vya ufisadi na mapendeleo vimeongezeka
sana.
Makundi yaliyoandaa maandamano hayo yamekuwa yakitumia
kitambulisha mada #zumamustfall kutafuta uungwaji mkono mtandaoni.
Maandamano hayo yamefanyika Siku ya Maridhiano, siku
ya mapumziko ambayo lengo lake ni kuleta pamoja watu wa asili mbalimbali Afrika
Kusini.
Mwandishi wa BBC Karen Allen aliye nchini humo anasema
amekutana na mmoja wa walioshiriki maandamano dhidi ya utawala wa ubaguzi wa
rangi 1976.
Anasema maandamano hayo ni kama “mwanzo wa jambo”.
Amesema hiyo ni mara yake ya kwanza kushiriki maandamano
tangu wakati huo.
Bintiye mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nodel Askofu
Desmond Tutu naye amejiunga na wanaomtaka Rais Jacob Zuma ang’atuke.
Amenukuliwa na tovuti ya habari la DispatchLive
akisema: "Huwa twawachagua viongozi wetu na tunaweza kuwang’atua.”
Mpho Tutu ameambia mkutano mkubwa wa #ZumaMustFall
mjini Cape Town kwamba wanataka ufisadi nchini humo ukomeshwe.
Wakosoaji wa Rais Zuma wanasema ufisadi umezidi chini
ya utawala wake.
Amekanusha vikali madai hayo.
Leo Bw Zuma, akiongoza sherehe za kuadhimisha Siku ya
Maridhiano, ameahidi kukabiliana na ukosefu wa usawa miongoni mwa watu wa asili
mbalimbali.
Hakuzungumzia maandamano dhidi yake.
Post a Comment