Muhubiri kutoka Canada ameukumiwa kifungo cha maisha korea Hyeon
Soo Lim, 60, aliyekamatwa mjini Pyongyang baada ya kuzuru ta
ifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.”
ifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.”
Bw Lim, ambaye ni kiongozi wa Light Korean Presbyterian Church,
alikuwa ameenda kusaidia kituo cha kutunza wagonjwa, kituo cha kuwatunza watoto
na kituo cha kutunza mayatima.
Mhubiri huyo kutoka Korea, anadaiwa kukiri kuhusika katika njama
ya kupanga kupindua serikali na kuunda taifa la kidini.
Shughuli zozote za kidini ni marufuku nchini Korea Kaskazini.
Taifa hilo mara kwa mara huwakamata na kuwazuia wageni wanaoenda
huko kwa shughuli za kidini au kimishenari.
Bw Lim alihukumiwa baada ya kesi yake kuendeshwa kwa muda mfupi
na mahakama ya juu ya Korea Kaskazini.
Inadaiwa mhubiri huyo amekiri kutoa mihadhara na kusema “Korea
Kaskazini inafaa kusambaratishwa na mapenzi ya Mungu”, na kusaidia Marekani na
Korea Kusini kutoa usaidizi kwa wanaotoroka Korea Kaskazini.
SOURCE BBC
Post a Comment