Watanzania
waonesha wazi kuwa magufuri amepata waziri mpya na si mwingine ni naibu waziri
wa ofisi ya
waziri Mkuu, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jaffo amewatangazia
kihama wakurugenzi wote nchini watakaoshindwa kuwasimamia wakuu wa idara katika
Halmashauri zao.
Naibu huyo alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara yake
ya kikazi ya kwanza ya kushtukiza katika wilaya ya Bahi iliyopo mkoani
Dodoma.
Mbali na hilo ametoa muda wa siku 27
kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatumia mfumo wa kielektroniki kwa
ajili ya kukusanya mapato katika halmashauri husika.
Jaffo amesema kwamba kutokana mfumo
wa kizamani wa ukusanyaji mapato unachangia kwa kiasi kikubwa cha
watumishi wengi pamoja na wakurugenzi kufanya ufisadi na kupiga fedha ya Umma.
Katika hatua nyingine amewaagiza
watumishi wote katika halmashauri ya Bahi pamoja na halmashauri nyingine nchini
kuhakikisha hawakai maofisini na badala yake watembelee miradi na kujua
matatizo ya wananchi.
Amesema hakuna haja ya watumishi
kukaa maofisini kwa ajili ya kusubiri taarifa ambazo wakati mwingine ni za
upotoshaji na kusababisha wananchi kuichukia serikali yao.
Katika ziara hiyo Jaffo
yaameshangazwa na Halmashauri ya wilaya ya Bahi iliyopo mkoa wa Dodoma kutokuwa
na takwimu sahihi za kazi zao.
Mbali na hilo ameishukia idara ya
utumishi kwa madai kuwa wakuu wa idara hiyo wamejigeuza kuwa miungu watu jambo
ambalo linachangia kuwepo kwa viashiria vya rushwa kwa watumishi wa kada ya
chini.
Hali hiyo ilibainika kutokana na
ziara ya kwanza ya kushtukiza iliyofanywa na Jaffo kwa lengo la kutaka
kujua ni jinsi gani utendaji unafanyika wilayani hapo.
Katika ziara hiyo Jaffo alishuhudia
ambavyo watumishi 38 ndiyo waliowahi kazini kati ya watumishi 110.
Akizungumza na watumishi pamoja na
wakuu wa idara alisema umefika wakati wa watumishi kuacha kazi kwa Mazoe na
badala yake wafanye kazi kulingana na mahitaji ya sasa.
“Katika idara ya utumishi kuna
matatizo makubwa zaidi jambo baya zaidi ni watumishi kujifafanya miungu watu
kwa watumishi wa kada ya chini.
“Utashangaa mkuu wa idara ya
utumishi anavyowafanyia roho mbaya watumishi wenzao kwa kutoshughulikia malipo
yao au upandishaji wa vyeo huku akiwa na malengo ya kutaka rushwa.
“Katika hatua nyingine watoto wa kike
wanajikuta katika wakati mgumu zaidi ikiwa ni pamoja na kufanya mambo mabaya
kututokana na usumbufu ambao unafanywa na wakuu hao wa idara,” amesema Jaffo.
Katika hatua nyingine ameutaka
uongozi kutoa maelezo ni kwanini wenyeviti wa serikali za mitaa kutofanya
mikutano ya kisheria kwa ajili ya kuwasomea wananchi mapato na matumizi katika
maeneo yao.
“Inashangaza kuona jinsi wenyeviti
waliochaguliwa na wananchi wasivyowatendea haki wananchi kwa kutowasomea mapato
na matumizi ndani ya mwaka mzima,” amesema Jaffo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
Halmashauri ya Bahi, Rachel Chuwa amesema watumishi watafanya kwa maelekezo ya
Naibu waziri.
Mbali na hilo amesema tatizo kubwa
katika wilaya hiyo ni ukosefu wa maji ya uhakika jambo ambalo ni tatizo kubwa
kwa watumishi na wananchi kwa ujumla.
Amesema serikali inaombwa kutoa
fedha kiasi cha Sh. 400 milioni kwa ajili ya kufanya mradi wa maji.
Naye mkuu wa wilaya hiyo, Francis
Mwongo amesema atahakikisha anasimamia maelekezo kwa kushirikiana na watumishi.
Post a Comment