Lile lilotarajiwa na wengi limetimia ilikuwa ni kutimiza sharia Mgombea
Ubunge w
a Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Arusha Mjini, Mh
Godblees Lema ameibuka Mshindi na kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Katika uchaguzi huo ulioshirikisha vyama vitano vya Siasa Mh
Lema amepata kura 68,848 kati ya kura 104,353 zilizopigwa sawa na asilimia 65.9
akifuatiwa na Mgombea wa CCM Bw Philemon Mollel aliyepata kura 35.907 sawa na
asilimia 34.4.
Wagombea wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Pamoja na
Navo Mollel wa ACT Maendeleo aliyepata Kura 342 sawa na asilimia 03, Zuberi
Mwinyi wa CUF aliyepata kura 106. Sawa na asilimia 0.1, na Makama Rashidi wa
NRA aliyepata kura 43 sawa na asilimia 0.04.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo Bw Juma Iddy,
jimbo la Arusha wapiga kura walioandikishwa ni 317.814, na waliojtokeza kupiga
kura ni 105,800 sawa na asilimia 32.83 na kura halali ni 104,353.
Post a Comment