Dk Magava amekuwa mtu wa kumi kukamatwa na polisi katika kampeni za jeshi hilo kudhibiti uhalifu chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema Dk Magava alikamatwa akiwa Sumbawanga na alirudishwa mkoani Iringa.
Mjengi alisema Septemba 15, mwaka huu walipata taarifa kuwa mhadhiri huyo anatumia mitandao ya kijamii kumkashfu Rais. Alisema waliamua kumsaka na walipopata taarifa kuwa Dk Magava amekwenda Sumbawanga waliwasiliana na polisi wa huko wakamkamata na kumrudisha Iringa.
Hata hivyo, Kamanda Mjengi hakuyataja maneno aliyotumia Dk Magava kumkashfu Rais kwa madai kuwa bado wanaendelea na uchunguzi na kwamba ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Kamanda Mjengi aliwatahadharisha wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuitumia kwa ajili ya maendeleo na si kutukana wala kukashfu viongozi au watu wengine.
Watu mbalimbali wamekuwa wakikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kumkashifu Rais au jeshi la polisi.
Related Posts
NCHI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE IMEZUKA KANANGA
Ghasia za siku mbili katika mji wa Jamhuri ya kidemorasi ya Congo zimesababisha vifo vya watu 10.[...]
Sep 24, 2016CUF WAJIBU BAADA YA LIPUMBA KUTANGAZWA KUWA MWENYEKITI
Baada ya kupokea Ushauri huo, The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kinapenda kueleza[...]
Sep 24, 2016LIPUMBA APEWA WENYEKITI CUF
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema kuwa Prof. Ibrahim Lipumba bado[...]
Sep 24, 2016KWA USHUJAA HUU CHADEMA WANATAKIWA KUIGWA
September 19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Temeke kimemfukuza uanachama[...]
Sep 24, 2016VIONGOZI WA DINI WA WASHAMBULIA CHADEMA
Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza viongozi[...]
Sep 24, 2016JAKAYA MRISHO KIKWETE AZIDI KUNG'ARA KIMATAIFA
Shirika lisilo la Kiserikali laSpeak Up for Afrika &nb[...]
Sep 24, 2016MADEREVA WA MALORI WALIOTEKWA NYARA KONGO WAOKOLEWA NA VIKOSI VYA JESHI
Madereva wa malori kutoka Tanzania waliokuwa wametekwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya[...]
Sep 16, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.