Vikosi
vya usalama Kananga vimekabiliana na wapiganaji wanaotaka kulipiza kisasi
mauaji ya kiongozi wao aliyeuawa na jeshi mwezi Agosti, maafisa na vyombo vya
habari vinasema.
Wanamgambo
hao waliushambulia uwanja w
a ndege wa mji huo Ijumaa na kumuua mfanyakazi mmoja
wa ndege, walioshuhudia wanasema.
Congo
imekabiliwa na ghasia za miaka kadhaa na ukosefu wa utulivu kisiasa.
Maandaamano
dhidi ya rais Joseph Kabila katika mji mkuu Kinshasa mapema wiki hii
yamesababisha vifo vya watu 50, Umoja wa mataifa unasema.
Ripoti
zinaarifu kuwa wapiganaji wanaomtii kiongozi wa kikabila aliyeuawa, Kamwina
Nsapu, waliingia katika mji wa Kananga Alhamisi asubuhi.
Kituo
cha Redio Okapi kinasema wanamgabo hao wamepambana na vikosi vya usalama na
hatimaye walitimuliwa.
Walirudi
Ijumaa na kukivamia kituo hicho cha ndege.
"Kulikuwa
na mapigano makali yaliohusisha silaha ndogo na kubwa," anasema Killy
Ilunga, aliyeuona mwili wa mfanyakazi wa ndege baada ya kuuawa.
"Waliingia
katika ukumbi wa uwanja wa ndege. Mmoja wao alimpiga kwa rungu."
Idadi
ya waliouawa haijathibitishwa, lakini ripoti zinasema idadi huenda ikawa kati
ya watu 10 na 13.
Msemaji
wa serikali Lambert Mende anasema hali imedhibitiwa.
Post a Comment