Askofu mmoja wa kanisa la kianglikana nchini
Uingereza amekuwa wa kwanza kutangaza h
adharani kuwa anashiriki mapenzi ya
jinsia moja na sasa yuko kwenye uhusiano.
Kasisi
Nicholas Chamberlain, amesema kuwa walioshiriki katika mchakato wa kumteua
mwaka uliopita walialewa fika mwelekeo wake wa jinsia.
''Watu
wanajua nashiriki mapenzi ya jinsia moja, lakini si kitu cha kwanza nachoweza
kumwambia yeyote. Jinsia ni sehemu ya yule niliye, lakini ni kazi yangu ya
kitume ambayo ninataka kuiangazia ."
Watu wanajua nashiriki mapenzi ya jinsia moja,
lakini si kitu cha kwanza nachoweza kumwambia yeyote. Jinsia ni sehemu ya yule
niliye mimi, lakini ni kazi yangu ya kitume ambayo ninataka kuiangaziaNicholas
Chamberlain, Asakofu
Nicholas
Chamberlain anasema hata hivyo anafuata kanuni za kanisa zinazosema kuwa
haruhusiwi kuoa.
Msemaji
wa kanisa la England amesema: "Nicholas hajamkera yeyote na amekua wazi na
mkweli ukiuliza. Suala lake si la siri, ingawa ni la kibinafsi kama ilivyo kwa
wale walio katika mahusiano ya kimapenzi ."
Inadhaniwa
kuwa hakuna askofu yeyote anayehudumu aliyewahi kutangaza hadharani msimamo
wake wa kingono.
Kanisa
la kianglikana kote duniani limegawanyika sana miaka ya hivi karibuni kuhusu
masuala yanayohusu mwelekeo wa kijinsia na kutawazwa kwa makasisi walio katika
mapenzi ya jinsia moja.
Source BBC
Post a Comment