Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali
maombi mawili yaliyopelekwa kortini kupinga matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Bunda
mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana,
Maombi hayo yalipelekwa na wapiga kura wanne,
Magambo Masato na wenzake watatu dhidi ya Ester Bulaya (Chadema).
Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2015,
maombi hayo yalipelekwa na wapiga kura hao, kumtetea aliyekuwa mgombea ubunge
wa jimbo hilo, Steven Wassira kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwenye
uchaguzi huo Wassira aliangukia pua.
Uamzi huo umetolewa jana na Jaji Lameck
Mlacha, baada ya kupitia hoja zilizotolewa na Bulaya kupitia wakili wake, Tindu
Lissu kupinga kupokelewa kwa maombi ya wapiga kura hao.
Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida
Mashariki, aliweka mapingamizi matatu ambayo ni kukosewa vifungu vya sheria vya
kupeleka maombi kortini na kifungu cha 10, A na B ambavyo havijatolewa maelezo
ya kutosha.
Pingamizi lingine ni kifungu cha 11
kinachotaja vitendo vya rushwa vilivyofanywa na mfuasi wa Bulaya katika maelezo
ya wapeleka maombi hao lakini hawajavionesha licha ya kumtaja mfuasi huyo.
Katika maelezo ya Lissu kortini hapo,
alidai kuwa katika hoja ya kwanza ya kukosewa vifungu vya sheria kwamba,
vimekosewa na haviipi mahakama nafasi ya kutenda haki na mteja wake kutafuta
ushahidi.
Pingamizi la pili Lissu, alidai limekiuka
sheria na hakuna maelezo ya kutosha huku hoja ya tatu ikipigwa chini kwa maana
sheria haimtambui mfuasi bali anayetambuliwa ni mgombea (Bulaya) ama wakala
wake ambao wangetajwa ubunge ungeweza kutenguliwa.
Jaji Mlacha akitolea uwamzi mapingamizi
hayo alidai kuwa, kufuati kupitia hoja za pande zote mbili zilizotolewa Agosti
17 mwaka huu, anakubaliana na Lissu kwa kufuta hoja ya kwanza na tatu.
Jaji Mlacha amesema kuwa, pingamizi la
pili lililokuwa limewekwa na Bulaya kupitia wakili wake Lissu, anakubaliana
naye katika baadhi ya vipengele ambavyo ni pamoja na wapeleka maombi kushindwa
kutoa maelezo ya kutosha huku akitoa nafasi ya kuendelea kusikilizwa kwa kesi
hiyo.
“Paragraph (Aya) ya 11 ilitakiwa kusema
vitendo vya rushwa ambavyo vimefanywa na mfuasi wa Bulaya (Emmanuel Nteleja) na
mgombea (Bulaya) akiwa anafahamu vitendo hivyo licha ya hivyo, aya hiyo ina
mapungufu.
“Pamoja na hayo tayari uwamzi katika
pingamizi la kwanza lililokuwa likibishaniwa tayari Jaji Gwae (Mohamed Gwae)
alishalitolea uwamzi na nanuku maelezo yake;
“Mwombaji lazima aoneshe ameleta maombi
kwa kifungu gani na sheria gani ili kuirahisishia Mahakama katika kutoa
maamzi,” alinukuu Jaji Mlacha.
Jaji Mlacha amesema kuwa, kuna baadhi ya
vifungu ambavyo vinaipa mahakama nafasi ya kuendelea kuisikiliza kesi hiyo,
huku akidai kwamba, kesi hiyo itapangiwa siku na Jaji mwingine wa kuisikiliza.
Wakati maamzi hayo yakitolewa kortini
hapo, upande wa mjibu maombi namba moja uliwakilishwa na Wakili Onyango Otieno
huku mlalamikaji ukiongozwa na Wakili Constantine Mtalemwa.
source Mwanahalisi
Post a Comment