Cyril Ramaphosa alielezea kwamba mipira hiyo ya kondomu ilitengezwa kufuatia
malalamishi kwamba kondomu za serikali zilikuwa zina harufu mbaya na kelele.
Tangazo hilo la Ramaphosa lilizua hasira na tabasamu kutoka wanachama wa ANC
na kelele kutoka kwa upinzani wa chama cha EFF huku baadhi ya wanachama wake
wakisema ''mpatie Zuma hizo''.
Matamshi hayo ya wanachama wa EFF yanatoka miaka 10 iliopita wakati bwana
Zuma alipokiri kwamba katika kesi yake ya ubakaji ,alifanya mapenzi bila
kutumia mipira ya kondomu na mwanamke aliyekuwa na virusi vya HIV.
Aliondolewa mashtaka hayo lakini kukiri kwake kulizua mshangao mkubwa nchini
humo ambapo takriban watu milion saba wana virusi.
Source bbc Swahili
Post a Comment