UMOJA
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema hakuna haja ya
mazungumzo, majadiliano wala mijadala inayostahili kufanyika kati ya
Serikali ya CCM na Chadema na amemuomba Rais Dk John Magufuli kuendelea
na mikakati yake ya kisera ili kuimarisha uchumi.
Pia
umoja huo umeeleza kuwa dunia inajua, ulimwengu unaaelewa na Chadema
wanafahamu kuwa Tanzania hakuna mgogoro wa kisasa zaidi ya serikali
kupigania mabadiliko, nchi kuwa ya viwanda na kutokomeza maadui
umasikini, ujinga na maradhi.
Msimamo
huo umetolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka,
katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa White
House Makao Makuu ya CCM Mkoani hapa.
Shaka
alisema UVCCM ilijua, ilielewa na kutambua mapema Chadema na viongozi
wake walikuwa wakifanya maigizo katika siasa, hawakuwa na ubavu wala
jeuri ya kuandamana kwa madai aliyoyaita ni ya kipuuzi ambayo hayana
msingi kwa mustakabali wa nchi na maendeleo yake.
Alisema
viongozi na wafuasi wa Chadema walishindwa kuandamana Septemba Mosi,
hawataweza na wala hawatajaribu kufanya hivyo Oktoba Mosi kwa sababu
wanachotaka kukifanya ni utoto wa kisiasa baada ya kushindwa kubuni
mkakati wa kukiendesha chama chao ili kiaminike na kukubalika.
"Tunazo
habari wabunge wa Chadema wamechachamaa na kumbana Mbowe kwa hoja
wakitaka kurudi bungeni ili kushiriki vikao kwa kuwa hawaeleweki kwa
wapiga kura wao majimboni lakini pia wanakabaliwa na 'waya mkali',
hawaoni kwa nini wasishiriki vikao vya Bunge huku baadhi ya viongozi wa
juu wa chama hicho wakiwa na utajiri na wengine
wafanyabiashara,"alisema Shaka.
"Cha
ajabu hata na wale wazee tuliokuwa tukiwaheshimu bila soni wanashiriki
kuudanganya ulimwengu wakitoa madai ati kuna mgogoro wa kisiasa
unaohitaji suluhu, yafanyike mazungumzo na majadiliano,"alisema Shaka.
Alisema
UVCCM imeshangazwa na madai ya Chadema na kusema kwamba chama hicho na
viongozi wake wamekuwa wakikutana na viongozi wa madhehebu ya dini na
mashirika ya kiraia, kisheria yaliyowataka ati wasiteshe maandamano kwa
muda hadi Oktoba Mosi mwaka huu.
"Tumekuwa
tukijiuliza bila kupata majawabu ya kina pale Mbowe na Chadema
wanaposema wameshauriwa na viongozi wa madhhebu ya dini na taasisi
zingine. Je hapo awali pia walishirikiana na viongozi hao kupanga na
kuitisha maandamano yenye lengo la kumdhihaki Rais na kumwita dikteta?"
alihoji Kiongozi huyo wa Vijana.
Hata
hivyo, alisema si jambo linaloingia akilini na mtu alazimike kuyamini
maneno ya Chadema kama kweli viongozi wa dini na taasisi zilizotajwa,
walihusika na kushiriki mpango wa uitishji maandamano ya vurugu na sasa
wahusike tena kuwakataza Chadema wasifanye maandamano.
"UVCCM,
wananchi wema, wapenda amani na utulivu, viongozi wa mashirika ya
kiraia na madhehebu ya dini, hatuwezi kusimama hadharani kuitbitishia
dunia kama Tanzania kuna mgogoro wa kisiasa unaohitaji yafanyike
mazungumzo, majadiliano hadi kufikia mapatano," alieleza Shaka.
Alisema
ulimwengu mzima unafahamu, mashirika na jumuia za kimataifa nazo
zinaelewa kwamba katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana,
wananchi walitekeleza wajibu wao wa kikatiba na kupitia demokrasia ya
uchaguzi walimchagua kwa kura Rais Dk. Magufuli kuwa Rais wao na
matokeo ya uchaguzi huo yalitangazwa na chombo chenye dhamana ya
kisheria na kikatiba ambacho ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Shaka,
alisisitiza kuwa wananchi wote, mashrika ya Kimataifa na ulimwengu
unaelewa Dk. Magufuli baada ya kuchaguliwa, serikali yake bila kupoteza
wakati imekuwa ikihimiza kwa nguvu zote mpango wa uwajibikaji,
utendaji wenye ufanisi, nidhamu, huku serikali yake ikipiga vita
ufisadi, ubadhirifu wa mali za umma pia ikikusanya kodi na kuongeza
mapato ya taifa.
"Chadema
na UKUTA wao wanachotaka ni siasa za mitaani na maandamano haramu.
Wanataka kukithiri kwa malumbano na mabishano yasiyo na maana badala ya
wakulima, wafanyakazi, wavuvi na wafugaji wafanye kazi kwa bidii,
kujituma ili wazalishe mali na kujienga uchumi na kimaendeleo
alisema,"alisema Shaka .
Shaka
alieleza kuwa haipendezi na haiwapi hadhi au heshima mbele ya jamii
watu wanaojiita viongozi wa kisiasa wa Chadema kuwa na uhodari wa
kutunga uongo, wakauamini, kuueneza na kuutetea kwa misuli ya unafiki na
upotoshaji.
"UVCCM
tunawaasa viongozi wa Chadema waache mara moja siasa za utoto na tabia
ya kuwatia hofu wananchi, wasiwafanye waishi kwa wasiwasi kwa siasa zao
uchwara ambazo zimekosa afya na wala haiwapi heko au heshima mbele ya
dunia,"alisema Shaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment