0
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es laama aliyebobea katika fani ya sayansi ya jamii Dk Bashiru Ally amemtaja Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM  Shaka Hamdu Shaka kama ni mwanasiasa kijana anayechipukia, akijiamini na kujituma kwa bidii.

Amesema viten

do vyake, matamshi, ufafanuzi au anapojaribu kutoa maelezo na majibu aidha binafsi au kwa niaba ya jumuia anayoiongoza yanadhihirisha kama aliyejawa na dhamira ya kutenda mambo mengi makubwa.

Dk Bashiru ameeleza hayo jana katika mafunzo elekezi kwa watendaji wa uvccm ngazi za wilaya na mikoa toka mikoa sita ya kanda ya ziwa yaliofanyika kwwnye uwanja wa ccm kirumba mkoani hapa.

Dk Bashiru alisema ingawaje maneno ya mtu mara zote  hayawezi kuchukukiwa kama kielelezo na ithbat ya moja kwa moja ila amemtaja kiongozi huyo kama aliyeanza kwa mguu mzuri katika uga wa siasa.

Alisema kwanza anaonekana kuishi kwa kuyatazama mahitaji ya  wakati kisiasa, anayesoma alama za nyakati na mazingira ya kisiasa huku akijua anatoka chama tawala na kukioigania kiendelee kuongoza Taifa kwa ridhaa.

"Ulimi wa mtu aghalab hutoa matamshi mabaya au mazuri  lakini hupendeza matamshi yanapotoka yakandamana na vitendo halisi, kwa anavyoonekana Shaka ni kama aliyeshiba dhamira na kubeba matarajio toka ilipo jumuiya yake ili aiifikisha mbali zaidi"alieleza Dk Bashiru.

Aidha alisema haitoshikwa mtu mmoja, kikundi au watu fulani wakaonekaba ndiyo wenye kubeba dhamira, makusudio na mikakati huku wengine wakivunja wenzao matumaini, kutofanya kazi kwa bidii na kutojituma kimaatifa..

Msomi huyo aliwaeleza watendaji hao wa UVCCM kwamba  kazi za utendaji wa kitaasisi zinahitaji ari,  msimamo wa pamoja, ukamiloshaji wa mipango, sera namalengo kwa njia za ushirikiano na mahusiano mema kila wakati.

"Mkiweka mbele maslahi ya chama chenu, uzalendo kwa nchi yenu, mkakataa kuwa waasi na wasaliti hamtajikwaa njiani kabla ya kufika mwisho au ukomo wa safari yenu , jambo muhimu ni mshikamano, upendo na kuhimiza mawasiliano ya utendaji "alisema

Akizungumzia baadhi ya watu wakiwemo na wanasiasa ambao hujijitutumua kwa madai ya kupigania mabadiliko huku wao wenyewe wakidhamiria kuvunja sheria na kukiuka katiba,alisema ndiyo wanaostahili kupewa majina ya udikteta.

Alisema ikiwa ni watu wa kawaida au wanasiasa ndiyo wanaolazimisha yatokee mambo kinyume na taratibu a kuheshimu misingi ya katiba na sheria ndiyo wenye viashiria  tosha vya kuitwa  madikteta si vinginevyo.

"Rais Dk Magufuli anaposema wakati wa kampeni na kisiasa umemalizika hadi mwaka 2020 na kwqmba sasa ni wakati wa kujenga uchumi hapo hajavunja taratibu , sheria na wala hakiuki katiba, chama chenye serikali ndicho linachotakiwa kutimiza ahadi zake za kisera kabla ya kuitishwa uchaguzi mwingine "alisema Dk Bashiru.

Hata hivyo alikitahadharisha chama cha mapinduzi kuwa makini na kukumbuka mtikisiko uliokikumba mwaka 2015 na kueleza kuwa bila ya umadhubuti wa chama hicho , misingi na viongozi wake kingepasuka au kugawanyika .

"Lilikuwa ni tetemeko kubwa na zito la kutengenezwa na watu, si tetemeko la kiasili lama lililotokea Kagera, ccm kingekosa kuwa na misingi yake kisingehimili misukosuko na dhoruba iliokikabili chama hicho hasa katika kumpata mgombea bora was urais "alieleza

Watendaji wa uvccm toka ngazi za wilaya na mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, shinyanga , Mara na kagera wamepata mafunzo elekezi ya siku tatu mkoani hapa.

Post a Comment

 
Top