Msimu wa ligi kuu England umekuwa mgumu sana kwa Cesc Fabregas tangua uanze amecheza mechi moja tu kati ya chelsea na Liverpool napo aliingia dakika za majeruhi na kuonesha kiwango kizuri katika uwanja wa Stamford Bridge am
bapo chelsea alipigwa 2-1, ikiwa chelsea imecheza mechi tano mpaka sasa
Kabla ya mchezo huo wa Ijumaa, alikuwa amecheza jumla ya dakika 26 na
kuongeza zingine sita na sasa amefikisha jumla ya dakika 32.
Kwa aina ya mchezaji kama Fabregas ambaye alikuwa sehemu muhimu
kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa EPL msimu wa 2014/15, hali hii
lazima imuwie vigumu sana.
Lakini bado anaonesha kuwa na moyo wa dhati wa kuendelea kutoa
mchango wake klabuni hapo licha ya changamoto anazokutana nazo kwa sasa.
Amekuwa akifanya vyema pindi tu anapoingia uwanjani mfano mzuri ukiwa
ni kwenye mchezo dhidi ya Watford wakati alipotoa pasi safi ya goli la
ushindi wakati Chelsea ikiwa kwenye wakati mgumu.
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Fabregas aliandika hivi: “It hurts a
lot to be dropping points again but we must stand up strong and learn
from our mistakes.
+Thank you so much for the love.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment