hii ni taarifa ya kushtua kuhusiana na masuala ya afya, hasa kwa wakazi wa mijini. Ni kwamba mihogo ya kukaanga maarufu kama ‘chips dume’ ni miongoni mwa vyakula vilivyobainika kuwa vinaweza kuwa chanzo cha aina mojawapo ya maradhi ya kisukri (type 2 diabetes).
Aidha,
mbali na chips dume, vyakula vingine vyote
vinavyokaangwa kwa mafuta
vinaweza kuwa chanzo cha maradhi hayo ya kisukari endapo uandaaji wake
hautafanyika kwa kuzingatia tahadhari za kiafya.
Kwa mujibu
wa ripoti ya utafiti iliyotolewa hivi karibuni, ni kwamba vyakula
vilivyoandaliwa kwa kuchemshwa au kuivishwa kwa mvuke ndiyo pekee
vilivyo salama zaidi kwa sababu ya kutokuwa na tishio hilo la kisukari
kwa walaji, wakati mihogo, viazi na vyakula vingine vinapokaangwa au
kuokwa au kuchomwa hutoa kemikali iitwayo glycation.
Aidha,
kunapokuwa na kiwango cha juu cha kemikali hiyo, matokeo yake huwa
kunatokea ukinzani dhidi ya insulin kwa mlaji wa chakula husika na
matokeo yake ni uwezekano wa maradhi ya kisukari kwa mujibu wa ripoti ya
utafiti huo.
Kwa
kawaida insulin ni aina ya kichocheo (homoni) ndani ya mwili ambacho
husaidia kurekebisha kiwango cha sukari ambacho ni chanzo cha nishati
mwilini. Bila ya kuwa na insulin au kukiwa na ukinzani dhidi ya
insulini, kiwango kikubwa cha sukari hubaki kwenye damu. Hali hiyo pia
inaweza kusababisha matatizo ya moyo, macho, figo, na ogani nyingine
mwilini.
SOURCE NIPASHE
Post a Comment