Hatua ya serikali ya
kuwapatia hifadhi wageni hao ambao hawakuhukumiwa kwa kutekeleza uhalifu
wowote,imekosolewa na wengi nchini Ghana huku viongozi wa kikristo wakisema
kuwa huenda wakawa tishio.
Shirika la habari la
Reuters limemnukuu Mahama akisema kuwa raia yeyote wa Ghana anakabiliwa na
tishio la kufariki barabarani kwa ajali ikilinganishwa na tishio
linalosababishwa na wageni hao.
''Wanataka
kuanza tena maisha yao ili waendelea kuishi kama watu wa kawaida.hakuna la
kutuogofya''.
Awali mmoja ya wafungwa
hao wa Guantanamo ,Mahmud Umar Muhammad Bin Atef,amekiambia kituo kimoja cha
redio vile yeye na wafungwa wengine walivyoiunga mkono timu ya Black
Stars,wakati wa kombe la dunia la mwaka 2010.
source bbc
Post a Comment