Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano na
Mazingira), Luhaga Mpina, Meneja wa Mgodi huo, Asa Mwaipopo,
amesema gharama za kuendesha mgodi hazipo hivyo wanatarajia kutafuta
mwekezaji mwingine atakaendelea na shughuli ya uchimbaji.
Amesema kuwa ifikapo Juni mwaka huu shughuli za kuendelea na
uchimbaji (Mining) katika mgodi huo wa Buzwagi zitasimama na ba
dala yake
wataendela na uzalishaji wa maeneo ya akiba hadi mwaka 2019 watakapofunga rasmi
shughuli za uzalishaji.
“Hatutafunga kabisa mgodi huu ambacho tutafanya ni kusitisha
shughuli za uchimbaji (mining) kuanzia Juni, lakini ile akiba ambayo tulikuwa
hatujaigusa tutaendelea nayo mpaka 2019 na kuufunga moja kwa moja na kama kuna
mwekezaji mwingine atauziwa aendelee na uzalishaji,” amesema Mwaipopo.
Hata hivyo amesema sababu zilizopelekea mmiliki wa mgodi huo
kuacha kuendelea na uchimbaji ni kutokana na kiasi cha fedha kilichotumika
katika uwekezaji kuwa kikubwa ikilinganishwa na kibachozalishwa pamoja na
gharama za kuendesha mgodi kupanda.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais (Muungano na
Mazingira), Luhaga Mpina, amesema kuwa mwekezaji huyo amekomba dhahabu yote
katika eneo hilo na kuondoka nayo, hivyo hasara haitakuwa kwa mwekezaji huyo
bali itakuwa ni Taifa la Tanzania.
“Mmeondoa dhahabu yote alafu mnasema mnafunga mgodi hii ni
hasara kwa Taifa na sio kwenu, mimi nafahamu kabla ya kuwekeza lazima utafiti
wa wataalamu wenu ufanyike, hapa hakuna kufunga mgodi wala nini,” amesema
Mpina.
Mbunge wa Kahama, Jumanne Kishimba, amesema kuwa licha ya mgodi
huo kudai kwamba unaendesha shughuli zake kwa hasara lakini tatizo kubwa ni
matumizi makubwa ya fedha kwa watumishi wa mgodi huo wanaofanya kazi Kahama na
kuishi Dar es salaam.
“Kuna wafanyakazi wamegeuka miungu mtu katika mgodi huu, mtu
anafanya kazi hapa Kahama analala Dar es Salaam, anatumia usafiri wa ndege kuja
kazini unazani kuna faida watakayoipata kweli hawa,” amesema Kishimba.
SOURCE Mwanahalisi
Post a Comment