matokeo ya mitihani hiyo
iliyofanyika nchi nzima kuanzia Novemba, 16 hadi 27, Katibu Mtendaji wa Baraza
la Mitihani, Dk Charles Msonde amesema jijini Dar
es Salaam leo kuwa jumla ya
watahiniwa 164, 547 sawa na asilimia 89.00 ya watahiniwa wote wa kike
waliofanya mitihani hiyo wamefaulu.
Amesema watahiniwa 159,
521 sawa na asilimia 89.24 ya watahiniwa wote wa kiume waliofanya mitihani hiyo
nao wamefaulu huku wanafunzi 39, 567 sawa na asilimia 10. 88 wameshindwa
kukidhi viwango vya kuwaruhusu kuendelea na kidato cha tatu.
Akifafanua kuhusu matokeo
hayo, Dk Msonde amesema ufaulu umeshuka kwa masomo ya Uraia, Historia,
Jiografia, Kiingereza, Fizikia, Biolojia, Hisabati na ‘Book Keeping’
ikilinganishwa na mwaka 2014.
Amesema ufaulu umepanda
kidogo katika masomo ya Kiswahili, ‘Commerce’ na Kemia ikilinganishwa na ufaulu
wa masomo hayo mwaka 2014.
Ameitaja mikoa ya Mwanza,
Dar es Salaam, Mbeya na Iringa kuwa ndiyo iliyotoa shule kumi bora huku shule
kumi zilizofanya vibaya zikitoka mikoa ya Tanga Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.
Katibu huyo amesema jumla
ya wanafunzi 396, 770 waliandikishwa kwa ajili ya mitihani hiyo ya upimaji
ambapo 33, 104 sawa na alimia 8.3 hawakufanya mitihani hiyo nchi nzima kutokana
na sababu mbalimbali zikiwemo za utoro na maradhi.
Post a Comment