0
hayo huenda yakazidisha uhasama baina ya madhehebu mbalimbali eneo hilo. Idara ya mashauri ya kigeni ya Marekani imewahimiza viongozi wa eneo hilo kutia juhudi maradufu kupunguza mvutano.
Nchini Iran, waandamanaji waliokasirishwa na mauaji ya mhubiri huyo waliwasha moto majengo ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran.
Sheikh Nimr alikuwa miongoni mwa watu 47 wameua ka vitendo vya kigaidi 
Aliunga mkono maandamano dhidi ya utawala wa Saudi Arabia katika mkoa wa Mashariki wenye Washia wengi mwaka 2011.
Kupitia taarifa, msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni ya Marekani John Kirby ametoa wito kwa serikali ya Saudi Arabia kuheshimu na kulinda haki za kibinadamu.
Aidha, ameitaka Saudi Arabia kuhakikisha kuna haki na uwazi katika uendeshaji wa kesi.
Kuuawa kwa Sheikh Nimr kulisababisha maandamano maeneo ya Washia Mashariki ya Kati, na hasa Iran na Bahrain.
Awali, serikali ya Iran, inayoongozwa na Washia, na ambayo ni mpinzani wa Saudi Arabia inayoongozwa na Wasunni katika kanda hiyo, ilishutumu vikali mauaji ya Sheikh Nimr.
Wizara ya mashauri ya kigeni ya Iran ilisema ufalme huo wa Kisunni utalipia kitendo hicho.
Aidha, ilimwita balozi wa Saudi Arabia mjini Tehran kulalamika.
Kwa upande wake, Saudi Arabia ililalamikia balozi wa Iran kile ilichosema ni uingiliaji kati wa Tehran katika masuala ya ndani ya Riyadh.
Source BBC


Post a Comment

 
Top