Rais John
Magufuli adanganya umma na raia
watanzania kwa kubana matumizi, hayo maneno
si yangu bali ni ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk
Makongoro Mahanga amesema uwingi wa makatibu wakuu unakinzana na dhana ya yake
ya kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri.
Lakini
naibu waziri huyo kwenye Serikali ya Awamu ya Nne amesifu hatua mbalimbali za
kupambana na ufisadi anazochukua Rais Magufuli akisema amefanikiwa kutumbua
majibu, lakini sasa anatakiwa awe na ubunifu katika kutatua matatizo ya
wananchi.
Dk Mahanga
alikuwa Naibu Waziri wa Lazi na Ajira tangu mwaka 2008 na hakuwahi kuhamishwa
wala kupandishwa hadi ngazi ya uwaziri hadi Serikali ya Rais Jakaya Kikwete
ilipomaliza muda wake na baadaye kujiunga na Chadema.
Akizungumza
na Mwananchi jana, mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Segerea (CCM) alisifu kazi
inayofanywa na Rais Magufuli akisema inaonekana wazi.
“Kweli
ametumbua majipu ambayo hakika yalikuwa yameiva,” alisema Dk Mahanga.
“Naweza
kusema alikuta nyumba chafu na inanuka, ameisafisha. Sasa tunapenda kuona baada
ya kusafisha ataiweka katika hali gani? Atabuni nini ili kuwasaidia vijana
dhidi ya tatizo la ajira ili wengi waweze kumudu gharama za maisha.”
Lakini
katika waraka wake alioutoa kwenye mitandao ya kijamii, Dk Mahanga alimkosoa
Rais Magufuli akisema ameongeza ukubwa wa Baraza la Mawaziri baada ya kuteua
makatibu wakuu 27 wakati anawaaminisha wananchi kwamba wizara ni 15 tu.
Dk
Magufuli ameunda baraza lenye mawaziri 15, na manaibu waziri 19 na hivyo
kufanya baraza lake kuwa na jumla ya mawaziri 34, tofauti na baraza lililopita
lililokuwa na mawaziri 55. Uamuzi wa kupunguza idadi ya wizara ulikumbana na
changamoto ya nafasi za makatibu, ambao hata hivyo baadhi amewarudisha wizarani
ambako watapangiwa kazi na kubakiwa na makatibu 27.
“Si kweli
kwamba kapunguza ukubwa wa Serikali, bali kaongeza ukubwa wake. Sina hakika
kama wasaidizi wa Rais wamemshauri na kumweleza kwamba wizara si ofisi ya
waziri bali wizara ni ofisi ya katibu mkuu,” alisema Dk Mahanga akifafanua kuwa
katibu mkuu ndiye mtendaji mkuu wa wizara na afisa masuhuli.
Alisema
katibu mkuu ndiye mwenye dhamana ya utendaji na ndiyo maana hata katika ngazi
ya kata, ofisi inaitwa ofisi ya ofisa mtendaji wa kata na si ofisi ya diwani.
Kwa maana
hiyo, Dk Mahanga, ambaye kitaaluma ni mhasibu, alisema Rais alipounda Wizara ya
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, ambazo awali zilikuwa mbili tofauti na kuteua makatibu
wakuu watatu, kiuhalisia hakuunganisha wizara mbili kuwa moja bali ameunda
wizara tatu kutoka mbili za awali.
“Ongezeko
la gharama kwa kuongeza waziri mmoja ni ndogo sana kulinganisha na kuongeza
katibu mkuu mmoja. Waziri anapoteuliwa tayari anakuwa ni mbunge mwenye mshahara
wake wa ubunge na kinachoongezeka ni kama laki tano tu juu ya ule mshahara wa
ubunge na gharama nyingine ndogo za gari, pia mishahara na gharama za katibu
muhtasi, msaidizi na dereva,” alisema Dk Mahanga.
Alisema
kwa ujumla ahadi ya Rais Magufuli aliyotoa kwenye kampeni kwamba ataunda
Serikali ndogo, hakuitimiza badala yake ameongeza ukubwa wa Serikali.
Wakati wa
kampeni na alipoapishwa, Rais Magufuli alisema ataunda baraza dogo la mawaziri,
hiyo ilijenga shauku kwa wananchi kufahamu kiwango cha ukubwa au udogo wa
baraza hilo ikilinganishwa na mabaraza yaliyoundwa na watangulizi wake, tangu
Tanzania ipate uhuru mwaka 1961.
Dk Magufuli
pia alitoa ahadi hiyo alipozindua Bunge Novemba mwaka jana mjini Dodoma.
Post a Comment