0


Kwa mujibu wa Naibu Kamishna watu waliokamatwa wengi walio ingia bila vibali ni wachina na wa Ethopia kwa jijini Dar tu idadi kama ifuatavyo

Nchi hizo na idadi ya waliokamatwa kwenye mabano ni Nigeria (4), China (20), Ethiopia (23), Korea (9), Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoDRC (6), Somalia (3),Uganda (2), Madagascar (5), Burundi (2), Ivory Coast (1), Lebanon (1), India (1), Zimbabwe (1) na Ghana (1).

Hivi karibuni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipofanya ziara Makao Makuu Idara ya Uhamiaji, aliagiza ichunguze kampuni zote nchini zinazotoa ajira kwa wageni wakati ajira hizo wangeweza kupewa Watanzania wenye sifa.

Masauni aliwaambia watendaji wakuu wa idara hiyo kwamba lazima kuwe na mfumo thabiti wa kudhibiti tatizo hilo kwa ajili ya manufaa ya nchi nzima. 

Aliagiza idara hiyo kuimarisha ulinzi na ukaguzi wa mipaka nchini, kurahisisha mapambano dhidi ya wageni wanaoingia nchini kiholela.

Hata hivyo, alitaka idara hiyo kushughulikia haraka tatizo la vibali vya ukazi, kwa kile alichosema imebainika kuwepo wakazi wengi wa kigeni nchini waishio na kufanya kazi nchini kinyume na sheria za nchi

Post a Comment

 
Top