Bw Justice Wadyajena anadaiwa kutumia
“lugha ya matusi” dhidi ya mwanachama m
wenzake wa chama tawala cha Zanu-PF
aliyekuwa ameweka picha ya Bi Mugabe kwenye gari lake.
Kisa hicho
kinatazamwa na wengi kama sehemu ya vizozo ya ndani ya chama kuhusu nani
atamrithi Rais Robert Mugabe ambaye atatimiza umri wa miaka wa miaka 92
Februari.
Bw Wadyajena
amenukuliwa kwenye nyaraka za mahakama kwamba alimwambia Jimayi Muduvuri:
"Wewe ni mjinga sana, sawa na mama huyu wenu.” Atafikishwa kortini
Victoria Falls.
Mke wa rais
nchini Zimbabwe huitwa "amai", maana yake mama, na wafuasi wa chama
cha Zanu-PF.
Mbunge huyo
amekanusha madai hayo.
Post a Comment