Dk. Magufuli leo ametimiza siku 59 tangu kuapishwa kushika madaraka hayo Novemba 5, mwaka jana na ameshafanya mambo makubwa yaliyompa sifa kem kem kitaifa na kimataifa.
Kingunge ambaye mwishoni mwa
mwaka jana alikihama chama alichokiasisi cha CCM na kukitumikia kwa zaidi ya miaka 60, jana alisema kwa kawaida watu hupimwa utendaji wao wa kazi zinapofika siku 100.
mwaka jana alikihama chama alichokiasisi cha CCM na kukitumikia kwa zaidi ya miaka 60, jana alisema kwa kawaida watu hupimwa utendaji wao wa kazi zinapofika siku 100.
Kingunge ambaye alikuwa na kadi namba 8 CCM kabla ya kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi kumpigia kampeni aliyekuwa mgombea wa Chadema kwenye Uchaguzi Mkuu, Edward Lowassa, alisema ni mapema mno kujadili utendaji wa serikali ya Magufuli.
“Jamani nadhani ni mapema mno, msiwe na haraka nitatoa maoni yangu kuhusu utendaji wake muda huo utakapofika. Kwa sasa mwacheni afanye kazi zake msimwingie ingilie," alisema Kingune ambaye amewahi kushika nyadhifa nzito nzito serikalini.
"Kwani nyinyi mna haraka gani mpaka mnataka nitoe maoni yangu leo?"Aliuliza. "Bado ni mapema sana kumpima.”
Kingunge alisisitiza kuwa ni vyema Magufuli akaachwa afanye kazi zake kwa sasa.
Oktoba 4, mwaka jana, Kingunge alitangaza rasmi kujiengua ndani ya chama hicho, akisema alifanya hivyo kutokana na kile alichoamini kuwa CCM haifanyi yale yaliyoasisiwa na kujengewa misingi bora na waasisi wake.
Wakati akitangaza uamuzi huo, Kingunge alisema hakusudii kujiunga na chama chochote cha siasa nchini bali atakuwa mtanzania huru, lakini muda si mrefu akaungana na Ukawa kumnadi Lowassa.
Mwanasiasa huyo ambaye sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa CCM, alisema wananchi wanataka mabadiliko na wasipoyaona ndani ya chama hicho watayatafuta nje ya chama, ikiwa ni nukuu ya nasaha maarufu ya Baba wa Taifa, hayati Julius Nyerere aliyowahi kuitoa enzi za uhai wake.
Post a Comment