Maandamano hayo yanatokana na wasiwasi kwamba mpango wa kupanua
mji mkuu wa Addis Ababa na kuingia maeneo ya Oromia utawapokonya mashamba
wakulima wa Oromo.
Maafisa wa HRW pia wametoa wito kwa serikali kumwachilia huru
mwanasisa wa jamii ya Oromo aliyekamatwa mwezi uliopita.
Serikali imedai watu wanaoandamana wana uhusiano na makundi ya
kigaidi.
Mwezi uliopita, maafisa wa serikali walisema watu watano
waliuawa wakati wa makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama.
Maafisa kadha wa usalama, ambao idadi yao haikutajwa, pia
walifariki.
Post a Comment