0

Wakati vita dhidi ya wakwepa kodi katika Bandari ya Dar es Salaam ikipamba moto, umeibuka utata wa Sh bilioni 80 ambazo Waziri Mkuu Kas
sim Majaliwa, alisema ni kodi ya makontena 329 kutoka kwa wafanyabiashara 58, walioyatoa bandarini bila kuyalipia kodi.

Akitoa ufafanuzi wa ukusanyaji wa fedha hizo, Desemba 12, Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa wamekusanya Sh bilioni 10.6 kutoka kwa  wafanyabiashara 28 na kwamba wamebaki 15 wanaodaiwa Sh bilioni 3.7.

Kutokana na takwimu hizo, wafanyabiashara hao 15 nao wakilipa kodi, zitapatikana jumla ya Sh bilioni 14.3 kwa makontena yote 329, jambo linalofanya kuwe na upungufu wa Sh bilioni 65.7, tofauti na kiasi cha Sh bilioni 80 alichosema Waziri Mkuu Majaliwa.

Juzi Mkurugenzi wa Idara ya Elimu na Huduma kwa Walipakodi wa TRA, Richard Kayombo, alipotafutwa na gazeti hili kufafanua utata huo, alisema: “Sikiliza, usituingize kwenye ‘issue’ na waziri mkuu, ninachoweza kusema ni kwamba tumekusanya Sh bilioni 10.6 na zilizo nje bado ni Sh bilioni 3.7.”

Alipotafutwa Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Irine Bwire siku hiyohiyo, alisema waziri mkuu ameshatoka ofisini, lakini takwimu za Sh bilioni 80 hakuzitoa kichwani bali kwenye ripoti iliyotoka TRA.

“Mimi nitamuuliza vizuri kesho asubuhi (jana),” alisema Bwire.

Jana alipotafutwa tena, alisema hajafanikiwa kuzungumza na waziri mkuu kwa kuwa alikuwa na vikao vingi.

 “Labda baadaye kama atarudi ofisini kwa sababu sasa hivi amekwenda Ikulu kwenye kikao kingine,” alisema Bwire.

Rais Dk. John Magufuli, alipokutana na wafanyabiashara, alitoa siku saba kwa waliokwepa kulipa kodi kufanya hivyo na watakaokaidi watachukuliwa hatua.

Kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, Desemba 12, Dk. Mpango alisema ni kampuni 28 tu ndizo zilizotii agizo hilo la rais na kufanikisha ukusanyaji wa Sh bilioni 10.6.

Dk. Mpango alisema kuwa muda wa kulipa kodi kwa hiari uliisha Desemba 11, hivyo wafanyabiashara 15 ambao wameshindwa kulipa kodi katika kipindi hicho “wasubiri cha moto” kwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

“Hata hizo siku saba walizokuwa wamepatiwa tayari walikuwa wameshavunja sheria, hivyo wale waliolipa kwa wakati wamesamehewa kupelekwa mahakamani, lakini ambao hawajalipa watashtakiwa na kupigwa faini,” alisema Dk. Mpango bila kubainisha kiwango cha adhabu.

Alisema baadhi ya wafanyabiashara hao walienda “kulalamika”, lakini TRA haitawasamehe kwa kuwa kodi hizo zinahitajika kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Dk. Mpango alibainisha kuwa kati ya fedha zilizokusanywa katika kipindi hicho, Sh bilioni 4.16 zimetoka katika kampuni 13 ambazo zimelipa kodi yote iliyokuwa imekadiriwa, huku Sh bilioni 2.2 zikitoka katika kampuni 15 zilizotoa sehemu ya kodi wanayodaiwa.

Alisema bandari kavu (ICD) ya Azam ililipa kiasi cha Sh bilioni 4.17 kama dhamana kati ya Sh bilioni 12.6 ya kodi iliyokuwa imekwepa kulipa katika sakata hilo la upotevu wa makontena 329.
[6:57PM, 12/16/2015] ‪+255 787 820 007‬: MTANZANIA

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeridhia kutoa dhamana kwa watuhumiwa watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuwataka kila mmoja kutoa fedha taslimu Sh bilioni 2.6.

Akisoma uamuzi huo jana, Jaji Winfrida Koroso, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Tiagi Masamaki (56) ambaye ni Kamishna wa Forodha wa mamlaka hiyo, Burton Mponezya na Habibu Mponezya ambaye ni Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja.

Alisema kabla ya kutoa dhamana hiyo, mahakama hiyo imepitia maelezo ya pande zote mbili ambazo ni upande wa washtakiwa na wa Serikali ili kuangalia kama watuhumiwa hao wana vigezo vya kupewa dhamana.

Jaji Koroso alisema baada ya kupitia maelezo hayo, mahakama iliridhia kuwapatia dhamana hiyo, huku ikiwataka kutimiza masharti sita ili waweze kukidhi vigezo.

Aliyataja masharti hayo kuwa ni kila mwombaji kulipa fedha taslimu Sh bilioni 2.6 au mali yenye thamani ya fedha hizo na kudhaminiwa na wadhamini wawili ambao ni wafanyakazi wa Serikali wenye bondi ya Sh 20 kila mmoja.

Alisema, kila mwombaji hatakiwi kusafiri bila ya kibali cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako kesi hiyo inaendeshwa, kuwasilisha vibali vya usafiri ikiwamo paspoti katika mahakama hiyo na kuripoti mahakamani hapo kila baada ya wiki mbili siku ya Jumatatu.

Alisema masharti mengine ni kila mwombaji ahakikishe taarifa zote alizowasilisha mahakamani hapo ziwe zimesainiwa kisheria na kukamilisha taratibu za dhamana ndani ya saa 24 ili waweze kukidhi vigezo vya dhamana hiyo.

Awali, Masamaki na wenzake walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakituhumiwa kufanya makosa mawili ya uhujumu uchumi ambapo shtaka la kwanza ni kutoa makontena 329 katika Bandari ya Dar es Salaam bila ya kulipiwa kodi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 12.7.

Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa tarehe tofauti kati ya Juni mosi na Novemba 17 mwaka huu, sehemu isiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam, watuhumiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kuidanganya Serikali kuwa Sh bilioni 12.7 zimetolewa kwa kutoa makontena 329 katika bandari kavu ya Azam baada ya kodi zote kutolewa.

Shtaka la pili, inadaiwa kuwa Juni mosi na Novemba 17, mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam, walishindwa kutimiza majukumu yao kwa namna inavyotakiwa na kusababisha Serikali kupata hasara ya Sh bilioni 12.7.

SOURCE mwananchi

Post a Comment

 
Top