Aliyekuwa mgombea urais
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chini ya mwamvuli wa Umoja wa
Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa, anatarajia kufanya mkutano wa
hadhara kesho jijini Tanga, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kuwashukuru Watanzania
waliompigia kura w
akati wa uchaguzi mkuu.
Taarifa iliyotolewa kwa
vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
wa Chadema, Tumaini Makene, ilisema katika ziara hiyo Lowassa ataambatana na
viongozi wengine waandamizi wa Ukawa, ikiwa ni mwanzo wa ziara ya nchi nzima.
“Watawashukuru kwa namna
walivyounga mkono upinzani na ajenda ya mabadiliko katika uchaguzi mkuu
uliopita na wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani kuwa ndiyo nguzo
imara wanayoweza kuitegemea kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo
yao na ustawi wa taifa kwa ujumla.
“Itakumbukwa mbali ya
Watanzania kupiga kura za ushindi katika nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu
uliopita, wananchi waliwachagua wabunge wengi wa upinzani wanaotokana na Ukawa
na kuongeza nguvu kubwa ndani ya Bunge, hususan kupitia Kambi ya Upinzani
Bungeni,” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa
kambi rasmi ya upinzani bungeni itakuwa Serikali mbadala ya wananchi.
“Wameviamini vyama vyetu
hivyo kusimamia na kuongoza halmashauri zipatazo 34 nchi nzima, ikiwa moja ya
misingi imara katika kupigania mabadiliko ambayo Watanzania wanayataka,”
inasema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilifafanua
kuwa wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo ambayo ni ishara ya kuwa
matumaini yao kwa miaka mingine mitano yatasimamiwa na kuongozwa na upinzani
imara kupitia Ukawa.
Post a Comment