Raisi magufuri amtimua kazi mwenyekiti watakukuru na Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhi
sha kuwa
utendaji wa Takukuru chini ya Dk. Hoseah hauwezi kuendena na kasi anayoitaka.
“Eneo mojawapo la upotevu mkubwa wa mapato
ni Bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), lakini Rais
Magufuli (John) amesikitishwa na Takukuru kushindwa kuchukua hatua
yoyote,” amesisitiza Balozi Sefue.
Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema
Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja maafisa wanne wa Takukuru
ambao walisafiri nje ya nchi pamoja na kuwepo agizo la rais kuzuia safari za
nje ya nchi.
Watumishi hao waliosimamishwa kazi ni Mary
Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya
nchi licha ya kunyimwa kibali cha kusafiri kutoka kwa Rais au Katibu Mkuu
Kiongozi.
Post a Comment