Katika Bunge la
Tanzania, hivi majuzi kambi ya upinzani walionesha mchezo huo wa “mauzauza” au
“kiinimacho” mbele ya Rais wetu na viongozi kadha wa kitaifa.
Na kwa vile vyombo vya
habari vilitangaza na kuonesha vituko na viroja vyao, hali ilikuwa
dhahiri
shahiri. Viongozi wa genge la upinzani walisimama na kutaka Rais
halali wa Zanzibar Dkt. Shein eti asiingiye Bungeni kwa kudai kuwa
si Rais halali wa Zanzibar na muda wake wa uongozi umekwisha. Kama hilo
halitoshi, walionesha ujinga wao na ushenzi wao kwa kuzomea Bungeni
na kufanya fujo. Nia yao ni ilikuwa kumtetea Maalim kuwa ndiye aliyeshinda
wakati Tume ya Uchaguzi chombo halali hakijamtangaza. Maalim alifanya
makosa makubwa kwa kujitangazia ushindi wa Urais wa Zanzibar.
Nilidhani kambi ya upinzani
wakati wanasema Dkt. Shein siyo Rais halali wa Zanzibar basi na wakati huo huo
mshirika wao wa UKAWA Maalim naye angeandika barua rasmi ya kujiuzulu nafasi
yake ya Umakamo wa Kwanza wa Rais kwani na yeye muda wake umekwisha. Hawawezi
wapinzani kumtaka Dkt. Shein Rais wa Zanzibar aondoke Ikulu lakini
UKAWA wanapata kigugumizi cha kumwambia Makamo wa Kwanza na
yeye atoke Ikulu! Nilikuwa Zanzibar juzi, nilishtuka na kushangaa
nilipomwona Maalim amepanda gari yenye nembo ya serikali ya Zanzibar pembeni
mwa gari hiyo ipo bendera inapepea ya SMZ. Mbele ya gari ya Maalim ipo
pikipiki ya polisi na gari za polisi za Serikali ya Muungano. Nyuma
ya gari yake wapo askari na sare zao wameshika silaha za ulinzi.
Niliambiwa kuwa gari ile
ilikuwa inatokea ofisini pake Migombani ambayo imeandikwa Makamo wa Kwanza wa
Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mlangoni hapo ofisini
pake walinzi wake wakampa saluti ya nguvu ya heshima. Naye bila
kuchelewa huku akikenya akaipokea. Baada ya udadisi wangu nikaambiwa
bado anaishi katika jengo linalolipiwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar. Hata huduma za nyumbani kwake bado zinabebwa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar. Hata safari zake; za kwenda nje ya Unguja
kama Pemba na Dar es Salaam, ndege aitumiayo hulipwa na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar. Sina hakika kama mshahara wa mwezi wa Novemba kama atapokea au la!
Ni dhahiri bado anahudumiwa kiofisi na kimasilahi na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar. Analindwa na Serikali ya Muungano.
Nini tunajifunza?
Wanayoyasema UKAWA siyo wanayoyatenda. Kama bungeni walikataa Dr.
Shein asiingiye bungeni kwa sababu siyo Rais halali wa Zanzibar kwa nini hao
hao wasimtake Maalim aandike barua ya kujiuzulu umakamo? Kwa nini
wasimtake aache kuishi Ikulu, akataye ulinzi, asitumie gari la serikal na bendera? Kwa
nini asiache kutumia ndege za serikali na akitaka kwenda Pemba apande jahazi?
Hivi wale wabunge wa
kambi ya upinzani waliokuwa Dodoma si wanatakiwa wamwombe radhi Rais Magufuli,
Rais Shein na Watanzania kwa utovu wao wa adabu? Waombe radhi kwa
kuwadanganya Watanzania kusema kuwa Rais Shein siyo Rais halali wakati mshirika
wao wa UKAWA Maalim bado anang’ang’ania Ikulu na kufaidi huduma za
kimasilahi na ulinzi kwa fedha za walipa kodi?
Post a Comment