0
Wanajeshi wa Marekani waliofika nchini Libya wamelazimika kuondoka punde baada ya kutua, kutokana na masharti makali ya kundi la wapiganaji waliodhibiti eneo walilotua.
Duru zinasema kikosi cha wanajeshi 20 maalum waliokuwa wamejihami kwa silah
a za kisasa walitua katika uwanja mmoja wa kijeshi Magharibi mwa Libya Jumatatu ya wiki hii.
Msemaji wa idara ya jeshi la Marekani Barani Afrika{Africom} ameambia BBC wanajeshi hao waliamua kuondoka ili kuzuia vurugu.
Libya imekua kwenye machafuko tangu mwaka 2011 baada ya Kanali Muammar Gaddafi, kuondolewa madarakani.
''Wanajeshi hao wa Marekani walikwenda Libya kuimarisha uhusiano na jeshi la taifa'', ameongeza msemaji wa Africom Anthony Falvo.
Mwandishi wa BBC kaskazini mwa Afrika anasema kisa hiki ni aibu kubwa kwa Marekani ambayo ina maslahi mengi ndani ya Libya, hususan operesheni dhidi ya wapiganaji wa 'Islamic State'.
Libya ina serikali mbili; moja ina makao yake katika mji mkuu Tripoli na nyingine katika mji wa Tobrouk.
Wiki hii pande mbili zilisaini makubaliano nchini Morocco ya kuunda serikali ya muungano wa kitaifa.

Post a Comment

 
Top