Kumekuwa na wasiwasi kwamba wachafuko ambao yamekuwa yakiendelea nchini Burundi yanaweza kugeuka na kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe au hata mauaji ya kimbari.
Ijumaa iliyopita, watu 87 waliuawa kwenye mapigano katika mji mkuu Bujumbura, jeshi lilisema.
Wanachama wa Baraza la Amani na Usalama la AU wamekuwa wakikutana mjini Addis Ababa kujadili mzozo wa Burundi.
Adha, Balozi Mull K
atende kutoka Uganda amekuwa akiwapasha wanachama kuhusu hatua zilizopigwa kwenye mashauriano, Uganda ikiwa ndiyo mpatanishi wa kimataifa aliyeteuliwa na muungano huo.
Kikosi cha Akiba cha Afrika Mashariki pia kimeeleza wanachama kuhusu kujiandaa kwake kutumwa Burundi, hali ikibidi.
“Ujumbe wazi ambao umetoka kwa mkutano unaoendelea wa Baraza la Amani na Usalama, kwamba mauaji Burundi lazima yasitishwe mara moja,” ameandika Kamishna wa AU kuhusu Amani na Usalama Smail Chergui kwenye Twitter.
Machafuko yalianza Burundi Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza angewania kwa muhula wa tatu.
Serikali imesema hakuna uwezekano wowote wa kutoka kwa mauaji ya halaiki.
Awali, Kamishna wa Umoja wa Mataifa kuhudu Haki za Kibinadamu Zeid Ra'ad Al Hussein alikuwa amesema “Burundi imo kwenye njia panda, na kunaweza kutokea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe”.
Aliongeza kuwa kuna “matamshi ya kikabila” ambayo yameshuhudiwa kwenye mizozo ya awali Burundi.
Makabiliano kati ya Wahutu na Watutsi miaka ya 1990 yalisababisha vifo vya watu 300,000 nchini Burundi.
SOURCE BBC
Post a Comment