Home
»
kitaifa
»
News
» MAPENZI UPOFU MWANAUME AU MKE NA MTOTO NA YEYE AMEJINYONGA
mapenzi ni ugomvi na ugonjwa hii ni Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume
mmoja Mkazi wa kijiji cha Malolo Ndugu Chipunguli Mkisi (30) amemuua mke wake
kwa kumkata panga
kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi
amesema tukio hilo la aina yake limetokea Desemba 15 mwaka huu majira ya saa
7 mchana huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia, wilaya ya Mbozi, Mkoa
wa Mbeya.
Msangi amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo
ambaye ameuwawa na mumewe kwa kukatwa panga kichwani .
Kamanda Msangi amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya
mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume
mwingine.
inadaiwa kuwa baada ya tukio, mtuhumiwa alijinyonga kwa kutumia kamba kwenye
mti umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwake.
Aidha mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye vidole
na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa na maneno “kuwa
ameamua kumuua mke wake na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na
mahusiana ya kimapenzi na mwanaume mwingine aitwae kilasi nzowa”
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya vwawa. Ikiwa
uchunguzi bado unaendelea ….
|
Post a Comment