SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Mwanza,
limezilalamikia Taasisi za Serikali ikiwemo Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
ambazo zimekuwa sugu katika ulipaji wa ankara ya umeme kitendo kin
achosababisha
ukusanyaji mdogo wa kodi.
Manase amesema kuwa Taasisi za
Serikali zimekuwa sugu katika ulipaji wa ankara ya umeme kwa kutumia mgogo wa
Serikali huku Tanesco ikiendelea kupata wakati mgumu wa utoaji huduma kwa
wananchi.
Manase amesema Tanesco mkoa wa
Mwanza inahudumia jumla ya wateja 90,925 kati ya hao 81,487 wanatumia mita za
luku na 9,438 wanatumia mita za malipo, ambapo makusanyo kwa mwezi ni Sh. 6.4
bilioni.
Amesema licha ya kukusanya fedha
hizo kwa mwezi bado wanakabiliwa na tatizo la watumiaji wa umeme kushindwa
kulipa ankara zao kwani mpaka sasa wanazidai taasisi za Serikali na watu
wengine Sh. 3 bilioni.
Hata hivyo alizitaja Taasisi za
Serikali zinazodaiwa na Tanesco kuwa ni Jeshi la Wananchi Tanzania (TPDF) Sh.
809, 617 milioni, jeshi la Polisi, Sh. 515, 660, Magereza, Sh. 608, 306 na
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa) Sh. 347759.
“Mkuu wa mkoa (Magesa Mulongo)
tunapata wakati mgumu sana kuzidai hizi taasisi za umma hususani TPDF na Polisi
tunapoenda kuwadai na kuwaomba tuwafungie Luku, hawakubali sasa hali hii
imekuwa ngumu,” amesema Manase.
Aidha amesema Tanesco inakabiliwa na
tatizo la uchakavu wa vitendea kazi, uchakavu wa miundombinu ya usambazaji
umeme, wizi wa nyaya na nguzo, madeni katika taasisi na wizi wa umeme kwa
wateja unaofanywa na wateja.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa
Mulongo, aliwataka wafanyakazi wa Tanesco kufanya kazi kwa bidii kwani shirika
hilo limekuwa likilalamikiwa na wananchi kwa kushindwa kutoa huduma bora kwa
wananchi.
Mulongo amesema watu milioni 2.9
katika mkoa wa Mwanza wanahitaji huduma ya umeme lakini watumishi wachache
ambao ni wazembe katika kuwatumikia wananchi wameonekana kikwazo kwa Taifa.
“Jamii inahitaji utumishi wa dhati
na wanafahamu kibuli cha binadamu na watumishi wao, kama mtashindwa kufanya
kazi kwa dhati itakula kwenu kwa Serikali hii wengi wenu mtakuwa nje ya mfumo
wa ajira,” amesema Mulongo.
Post a Comment