MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amepinga hatua za
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwauwasa) kuongeza bei ya maji kwa
madai ongezeko hilo litasababisha wananchi wengi kukosa huduma.
Hivi karibuni Mwauwasa, ilitangaza
kuomba kuongeza bei ya maji kwa kile ilichodai kupanda kwa gharama za mita za
maji hivyo wanapendekeza
kuongeza bei ya maji kitendo ambacho wananchi wengi
jijini hapa walikipinga.
Mulongo akizungumza na wafanyakazi
hao amesema kuwa katika ufuatiliaji alioufanya amebaini kwamba kuna mchezo
uliandaliwa na mamlaka hiyo kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe na sio
wananchi hivyo haungi mkono hatua hizo.
“Mimi ninafahamu kwamba hawa watu
ambao mliwaleta na wakakubaliana na nyie kuongeza bei ya maji ni wa kwenu ambao
mliwaaandaa ili kuwaaminisha wananchi, sasa suala hilo siliungi mkono.
“Utaratibu wa kuongeza bei ya maji
ambao nyie mnadai kupanda kwa gharama za mita za maji kaeni muangalie upya
namna ambayo mtafanya,” amesema Mulongo.
Hata hivyo Mulongo aliwataka
wafanyakazi hao kuwajibika kwani ni wajibu wao kuhakikisha wananchi wanafikiwa
na huduma ya maji safi hususani wanaoishi katika maeneo ya miinuko.
Post a Comment