Makundi ya waasi ya kubaliana kusimamisha mapigano Hatua hiyo imefikiwa
baada ya kuwepo kwa m
kutano wa siku mbili mfululizo nchi Saud Arabia ambapo
makundi hayo ya waasi yalikutana kwa ajili ya mazungumzo ya awali.
Waasi hao kwa tamko moja
wamekubaliana kuweka silaha chini na kutoa nafasi
kwa majadiliano kuanza huku
sharti la kumtaka Rais wa Syria, Bashar Al Assad kuachia ngazi kabla ya
majadiliano hayo kuanza wakilifuta.
Awali makundi hayo yalitoa shatri
kwamba, ili kuweka silaha chini na kuingia kwenye mjadala ni lazima Rais Al
Assad ang’oke madarakani jambo ambalo rais huyo alilipinga na kueleza
haliwezekani.
Mkutano huo nchini Saudi Arabia
uliongozwa na mwenyekiti wake Abdulaziz Al-Sager ameeleza hatua gani itafuata
baada ya mazungumzo hayo.
Ameeleza kuwepo kwa mkutano ambao
utaamuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) Januari na kwamba utakua ni mkutano baina
ya upinzani na serikali ya Syria ambapo utachukua siku 10 za mwanzoni mwa
Januari.
Pamoja na hivyo, wapinzani wameeleza
kuwa Assad ataachia madaraka baada ya kutengeneza serikali mpya huku Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Nje nchini Marekani, John Kirbly akipongeza hatua hiyo
Post a Comment