0


   Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo imeeleza kuwa habari hizo sio za kweli na kueleza kuwa haijawahi kukwepa kodi na haihusiki kwa namna yoyote na makontena yaliyopotea bandarini.


Kuzaliwa
Dk. Magufuli ambaye kwa sasa ana miaka 56, alizaliwa Alhamisi Oktoba 29, 1959 Wilaya ya Chato mkoani Geita. Hiyo inamfanya kuwa siku muhimu sana kwake katika maisha.

Kushinda Urais
Alhamisi Oktoba 29, mwaka huu, wakati Dk. Magufuli akisherehekea siku yake ya kuzaliwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilimtangaza rasmi kuwa mshindi wa nafasi ya urais kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Kuapishwa Urais
Alhamisi Novemba 5, mwaka huu, Dk. Magufuli aliapishwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa mshindi Oktoba 29, mwaka huu.

Uteuzi wa mwanasheria mkuu
Baada ya kuapishwa Alhamisi Novemba 5, mwaka huu, siku hiyo hiyo alitinga Ikulu kwa mara ya kwanza akiwa Rais na kumteua George Masaju, kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, na kumuapisha siku iliyofuata.

Uteuzi wa waziri mkuu
Alhamisi Novemba 19, mwaka huu, Dk. Magufuli alipeleka rasmi jina aliloliteua la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, bungeni na siku iliyofuata akamuapisha na kulizindua Bung

Naibu Mkurugenzi Takukuru
Alhamisi Desemba 3, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli, alimteua Valentino Mlowola, kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Lilian Mashaka, aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Baraza la Mawaziri
Jana Alhamisi Desemba 10, mwaka huu, Rais Dk. Magufuli alitangaza rasmi Baraza lake la Mawaziri ikiwa ni siku 42 tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Kwa ujumla, matukio hayo yanaifanya siku ya Alhamisi kuzidi kuwa ya kipekee zaidi kwa Rais Dk. Magufuli kwani mbali ya kuonekana kuwa siku yake ya bahati, amekuwa akiitumia kufanya matukio makubwa ya kitaifa.


Post a Comment

 
Top