Waziri Mwigulu akutana na majukumu mazito ambayo labda tangu
aanze uwaziri hajawai kutana nayo ni baada ya mkulima mmoja ameuawa, mwingine
amejeruhiwa wakiwemo askari
polisi wawili kwenye mapigano dhidi ya
wafugaji wa kimang’ati kwenye kijiji cha Dihimba Turiani, mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa amesema mapigano hayo
yametokea baada ya wafugaji kutaka kuwachukua kwa nguvu ng’ombe zaidi ya 150
waliokuwa wakishikiliwa na wakulima kwenye ofisi ya kijiji hicho.
Mkwasa amesema siku ya tarehe 11 mwezi huu, mkulima mmoja
aliyejulikana kwa jina la Bakari Mulunguza alikuta ng’ombe zaidi ya 150 wakila
shambani kwake pasipo kuwa na mchungaji wa ng’ombe hao, ndipo Mulunguza
alipoomba msaada kutoka kwa wakulima wenzake kwa pamoja waliwaswaga ng’ombe hao
hadi kwenye ofisi ya serikali ya kijiji.
Amesema wakulima hao waliamua kuchukua uamuzi huo ili mwenye
ng’ombe ajitokeze na kupigwa faini kutokana na uharibifu uliosababishwa na
ng’ombe hao. Alisema siku iliyofuata ya tarehe 12, ndipo alipojitokeza mfugaji
mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Shaabani Ikeli na kudai kuwa yeye ndiye
mmiliki wa ng’ombe hao.
“Serikali ya kijiji ilimtaka mfugaji huyo kulipa faini ya
Shilingi laki mbili kama fidia kutokana na uharibifu uliosababishwa ; mfugaji
huyo alikubali na kuahidi kuwa angelipa faini hiyo, lakini cha kushangaza
alirudi na kundi kubwa la vijana wafugaji wakitaka kuwachukua ng’ombe kwa
nguvu, ndipo mapigano yalipotokea,” alisema Mkwasa.
Alimtaja aliyeuawa kuwa ni Mohamed Musa (43) mkulima wa
kitongoji cha Kaole, na aliyejeruhiwa ni Charles Paulo (35) ambaye amelezwa
hospitali ya Bwagala Turiani kwa matibabu.
Mkwasa amesema kitendo hicho kiliamsha hasira kwa wakulima ambao
walilipa kisasi kwa kuwakatakata miguu na sehemu mbalimbali za miili ng’ombe
150. Alisema polisi walifika eneo la tukio na kudhibiti vurugu hizo; amesema
polisi wawili wamejeruhiwa kweye mapigano hayo.
Mwigulu Nchemba Afika Afika Eneo La Tukio
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji Mh. Mwigulu Nchemba leo hii amefika katika eneo la tukio.Akizungumza na wananchi hao Waziri Nchemba alikuwa na haya ya kusema;
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji Mh. Mwigulu Nchemba leo hii amefika katika eneo la tukio.Akizungumza na wananchi hao Waziri Nchemba alikuwa na haya ya kusema;
"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, hakuna ardhi au mnyama mwenye thamani sawa na maisha ya mwanadamu yeyote yule,njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakulima na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na uongozi wa serikali wa eneo husika hatua kwa hatua".
Pia Mh. Mwigulu amesema ameagiza ulinzi maeneo yote yenye migogoro, pili wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia na kwa walio jeruhiwa, ameagiza wapatiwe matibabu kwanza bila kuchelewa na hatua za kisheria kwa wenye hatia zifuate.
"Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi, tunakwenda kuunda kamati za usuluhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria."
Post a Comment