Damu kikwazo shinyanga
ambapo imeonekana muda mwingi kutokuwa na damu
Mkuu wa Hospitali ya mkoa wa
Shinyanga, Dk. Ntuli Kapologweamesema kwa
mwezi mkoa unatakiwa kuwa na uniti 350 za damu lakini kabla ya kuanzishwa kwa
kampeni ya utafutaji wa damu zilikuwa zikipatikana uniti 20 jambo ambalo ni
hatari.
“Tatizo la
upatikanaji wa damu salama lipo wazi na wala halifichiki kutokana na hali hiyo
katika mkoa wa Shinyanga tumeanzisha kampeni ya upatikanaji wa damu sambamba na
kuanzisha mfuko maalum.
“Nimewashirikisha
wafanyakazi wa sekta mbalimbali, wafanyabiashara, mifuko mbalimbali ya kijamii
ili kuunga mkono juhudi za upatikanaji wa damu salama,” amesema Dk. Kapologwe.
Aidha Dk.
Kapologwe amesema baada ya kuanzisha mfuko huo wa damu kwa sasa wameweza
kukusanya uniti 200 za damu huku wakiwa na upungufu wa uniti 150.
Hata hivyo
amesema licha ya ukosefu wa fedha lakini bado kuna changamoto kubwa ya
upatikanaji damu ikiwa ni pamoja na jamii kutojitokeza kutoa damu.
“Unajua tatizo
la damu ni kubwa sana lakini jamii nayo haina elimu ya kutosha katika utoaji
damu mara nyingi wanaogopa unaweza kuona watu wakiwa kumi wameleta mgonjwa,
lakini anapofikia hatua ya kutoa damu wanaondoka kati ya hao kuni anatokea
mmoja.
“Hilo kama
halitoshi hata kada ya watumishi bado wana hofu ya utoaji damu utashangaa kuona
hawajitokezi katika utoaji damu,” amesema Dk. Kapologwe.
Kuhusu huduma
mahospitalini amesema ili huduma iwe nzuri zaidi ni vyema watanzania wengi
wakajiunga katika Huduma ya Mfuko wa Bima ya Afya.
Amesema jambo
lingine ni viongozi kufanya mambo kwa utekelezaji na ufuatiliaji badala ya
kutoa maagizo ambayo hayatekelezeki.
Post a Comment