Mfalme Buyelekhaya Dalindyebo alipatikana na hatia ya
kuteka nyara kuvamia na kuchoma moto makao ya watu.
Ameamrishwa kujiwasilisha kwa kituo chochote cha
polisi kilichoko karibu naye katika kipindi cha saa 48.
Chanzo chenye ukaribu na mfalme huyo kimeiambia BBC.
Dalindyebo ndiye mfalme wa kwanza kuhukumiwa jela
tangu Afrika Kusini ijipatie uhuru mwaka wa 1994.
Kesi hii inatokana na tukio lililotokea yapata mwongo
mmoja uliopita ambapo mfalme Dalindyebo anadaiwa kuwa alimteka nyara mwanamke
mmoja na wanawe 6 kisha wakachoma moto nyumba walimokuwa wakiishi.
Yamkini kosa lao lilitokana na mmoja wa jamaa wa
mwanamke huyo kukaidi amri ya kufika mbele ya mfalme huyo kujibu mashtaka dhidi
yake.
Mahakama ya kikatiba imekataa kusikiza rufaa yake.
Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani ambaye yuko
Johannesburg anasema kuwa ''Utawala wa mfalme huyo unasemekana kuwa ulikuwa wa
kiimla na unalaumiwa kwa mateso mengi yaliyowapata raia maskini katika maeno ya
mashambani.''
Utawala wake uliwaudhi wenyeji wengi na huenda asiwe
na wafuasi wanaompenda.
Aidha mwanamfalme Azenethi Dalindyebo ameratibiwa
kutawazwa kuwa mfalme endapo babake atafungwa jela.
Msemaji wa ikulu Daludumo Mtirara anasema kuwa kauli
ya mahakama ya kikatiba kukatalia mbali ombi la kusikizwa kwa rufaa ya kesi
hiyo imemnyima uwezo wa kikatiba wa kukata rufaa.
SOURCE BBC
Post a Comment