Lema si mbunge halali Arusha mjini hii inatoka na baad Aliyekuwa
mgombea ubunge wa jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CCM, Philemon Mollel
amepinga matokeo ya uchaguzi huo yaliyompa ushindi wa kishindo, Godbless Lema
wa Chadema.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya msimamizi wa uchaguzi
huo kutangaza matokeo, Mollel alidai kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa ambao
unafanya matokeo hayo kutokuwa halali.
Alisema kuwa wakati zoezi la kupiga kura likiendelea kuna gari
lililokamatwa likiwa na kura bandia za kumpa ushindi Lema ingawa alidai gari
hilo liliachiwa baadae.
“Kulikuwa na Noah ya diwani wa Chadema ambayo ilipita katika
baadhi ya vituo vya kupigia kura na kudai kupeleka vyakula. Lakini gari hiyo
tumeambiwa ilikuwa na kura za bandia zilizofanikiwa kuingizwa kwenye
masanduku,”alisema Mollel.
Kadhalika, alieleza kuwa kulikuwa na mapungufu makubwa kwenye
fomu za matokeo kwa kuwa baadhi ya fomu hazikuonesha idadi ya kura zilizopigwa.
Mollel alilirushia lawama jeshi la polisi kwa madai kuwa
liliwatisha akina mama na wazee kwenda kupiga kura.
“Hakukuwa na vurugu zozote, kwanini kuwatishia wanachi kwa
silaha na vifaa vya kivita,” alihoji Mollel.
Matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika
Jumapili, Disemba 13 yalimpa ushindi Godlbess Lema kwa kupata kura 68,848 sawa
na asilimia 65.9 huku Philemon Mollel akipata kura 35,607 sawa na asilimia 34
ya kura zote halali zilizopigwa na kuhesabiwa.\
Lakini watu wa arusha wanasema Lema ataakigombea mara hamsini
atashinda tuu
Post a Comment