MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea, amesema
atamshitaki Meneja wa Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani (UBT), Juma Idd, kwa
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, kutokana na kushindwa
kutatua kero zilizoko katika kituo hicho akifanya mazungumzo na
waandishi wa habari
Alisema mambo
waliyokubaliana na Meneja huyo ni pamoja na usafi katika eneo
hilo ikiwamo
kutengeneza mifumo ya kupitishia maji taka, kuzibua mitaro iliyoziba,
kuondoa madampo ya uchafu, kusafisha maeneo mengine machafu katika eneo
hilo pamoja na kero nyingine wanazozilalamikia wafanyabiashara.
“Wiki iliyopita nilitembelea kituoni hapa, pamoja na mambo
mengine nilikagua hali ya usafi na kusikiliza kero za wananchi, tulizungumza na
Meneja wa kituo tukakubaliana kwamba hizo kero zote atazifanyia kazi lakini
nimerudi tena kuangalia hakuna kilichofanyika,” alisema Kubenea na Kuongeza:
“Nimefika ofisini kwa Meneja lakini hajaniruhusu niingie kumuona
ili tuzungumze nifahamu ni tatizo gani ambalo limekwamisha kero hizi
kutekelezwa, nimesimama sana mlangoni lakini hata waliokuwa nyuma yangu
wameruhusiwa kuingia kumuona mimi nimeachwa, ninachosema ni kwamba hajanidharau
mimi bali wananchi wa Ubungo.”
Aliongeza kuwa atafikisha kero hizo kwa bosi wake, na endapo
naye atashindwa kuzifanyia kazi inavyostahili, ataziwasilisha katika baraza la
Madiwani ambalo lina nguvu ya kuamua kumuondoa katika nafasi hiyo au laa pale
linapoona hatekelezi majukumu yake ipasavyo.
Hii imeonesha kwamba sio
kufanya ziara tu bali na kushitaki watuhumiwa na huo ni mwanzo tu
Post a Comment