Polisi wawili wamekufa Kenya baada ya kushambuliwa na al shabab
Tukio ilo lilifanyika mpakani mwa Kenya na Somalia katika mji wa
El Wak
Polisi hao wanaaminika kuwa ndani ya gari lao wakishika doria
katika barabara moja kabla yao kushambuliwa ghafla na
wapiganaji hao
Wawili kati yao walipoteza maisha yao huku wengine wawili
wakijeruhiwa vibaya.
Shambulizi hili la leo limetokea takriban kilomita 5 pekee
kutoka pahala ilikoshambulia basi ya usafiri wa umma mapema wiki iliyopita na
kuua watu wawili.
Vyanzo vya wapiganaji hao wa Al-Shabab pia vinadai kuwa
walitekwa gari la kijeshi.
Dai hilo halijathibitishwa.
Hapo jana mtu anayeshukiwa kuwa mpiganaji wa Al Shabaab aliuawa
alipokuwa akitega bomu la ardhini katika barabara hiyo yaLafey – El Wak.
Kenya
Kumekuwa na mashambulizi kadhaa katika kanda hiyo katika wiki za
hivi karibuni.
Kundi hilo linadaiwa kuwa limegawanyika kuwa mawili baada ya
baadhi yao kukubali kuungana na wanamgambo wa Islamic State.
Wapiganaji hao walijitangaza Gamadhere aka Kuno wanaiunga mkono
ISIS.
Mashambulizi haya yaliyochacha kwa mjibu wa Inspekta mkuu wa
polisi nchini Kenya Joseph Boinett yanalenga kuwaonesha wadhamini wao kuwa
wanauwezo wa kufanya masg=hambulizi ndani ya Kenya.
Na askari hao walitumwa na nchini Somalia 2011 ilikudhibiti
ugaidi
Post a Comment