KATIBU mkuu wa Bakwata Taifa, Seleman Lolila
amemkana Meneja wa shule za El-Hijra, Mashaka Kitundu, kwamba hausiki kwa jambo
lolote la kumkingia kifua pale anapolalamikiwa na wafanyakazi.\
Lolila alitoa kau
li
hiyo alipokuwa akizungumza kwa njia ya simu kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya
malalamiko ya watumishi na walimu wa shule za sekondari za El-Hijra na Jamhuri
kwa kutolipwa mishahara na stahiki zao kwa ujumla.
Lolila amesema hawezi
kumkingia kifua Kitundu na wala hahusiki kwa jambo lolote.
“Mimi nipo Dar es Salaam,
Kitundu ndiye anayelipa mishahara sasa mimi nitamkingiaje kifua mimi,” amesema
Lolila.
Watumishi kwa nyakati
tofauti wakizungumza kwa masharti ya kutokutajwa majina yao walisema Kitundu
amekuwa akiwanyanyasa watumishi huku akitumia jina la katibu mkuu Bakwata
Taifa.
Kutokana na hali hiyo
watumishi na walimu wa shule ya sekondari ya El- Hijra pamoja na
sekondari ya Jamhuri ambazo zinamilikiwa na Baraza Kuu la Waislam
(BAKWATA) wamemuomba Mufti wa Tanzania, Shekhe Abubakari Zuberi kumsimamisha
kazi Meneja wa shule hizo, Mashaka Kitundu na ikishindikana wametishia
kugoma.
Watumishi hao wamefikia
hatua hiyo kwa madai kwamba hawana imani na mkuu wa shule ya sekondari ya Hijra
na meneja wa shule ya Hijra na Jamhuri ambaye pia ni Kaimu katibu wa Bakwata
mkoa, Mashaka Kitundu kutokana na manyanyaso wanayoyapata ikiwa ni pamoja na
kutolipwa mishahara yao na stahiki nyingine.
Wakizungumzia adha
yanayopata watumishi hao wamesema ni kutolipwa mishahara yao huku Meneja huyo
akiendelea kujineemesha, kujenga nyumba ya kifahari na kununua magari.
Watumishi hao pamoja na
walimu walisema kwamba kwa sasa wana hali mbaya kwani hawajalipwa mishahara yao
na pale wanapodai wanapigwa kalenda.
“Tangu mwezi wa saba hadi
mwezi huu hatujalipwa mishahara, mara tunalipwa sh.10,000 na wengine wanapewa
sh.50,000 na hatujui ni za nini.
“Mbaya zaidi Meneja
Kitundu ametugawa watumishi kuwa wale ambao amewafanya watu wake wa karibu huku
wengine akiwa hataki hata kuwasikiliza,” amesema mmoja wa watumishi.
Wamesema tangu Kitundu awe
meneja katika shule hizo hali ya watumishi imekuwa mbaya lakini jambo la
ajabu ni matumizi kuwa makubwa tofauti na kipindi cha nyuma.
“Hivi karibuni alitumia
kiasi cha sh. 800,000 kwa wiki kulisha wanafunzi wa Bweni ambao ni
kati ya 150 ambapo kawaida wanafunzi hao wa bweni utumia Sh. 450,000 kwa
wiki,” walieleza.
Katika msisitizo
watumishi walimuomba Mufti wa Taifa, Abbakari Zuberi kumwondoa au
kumsimamisha kazi ili uchunguzi ufanyike kubaini ubadhilifu alioufanya kwa muda
mfupi tangu afike shuleni hapo.
Katika hatua nyingine
watumishi hao wamesema Kitundu amekuwa akiwabeza watumishi kwa maelezo kuwa
hakuna mtu wa kumfanya lolote kwani yeye anamahusiano makubwa na Katibu mkuu wa
Bakwata Taifa, Seleman Lolila.
Hata hivyo watumishi na
walimu wamesema baada ya kumbana meneja aliwapatia kiwango sawa wote laki moja
kama sehemu ya kupunguza ukali wa maisha.
Kwa upande wake Meneja wa
shule hizo alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alisema suala la mishahara ni tatizo
lakini amelazimika kukopa benki na kulipa mishahara.
“Watumishi na walimu walikuwa hawajalipwa mshahara kwa
miezi mitatu lakini ni kutokana na ada kuchelewa hivyo nimelazimika kukopa
fedha kwa ajili ya kulipa mishahara ya miezi mitatu”alisema Kitundu.
SOURCE MWANAHALISI
Post a Comment