Uamuzi huo ulifikiwa baadaye Alhamisi baada ya mkutano mjini Addis Ababa.
Muungano
huo umep
anga kutuma walinda Amani 5,000 wa kulinda raia.
Umoja
wa Mataifa unakadiria watu 400 wameuawa tangu machafuko kuzuka mwezi Aprili
Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba angewania urais kwa muhula wa tatu.
AU
huenda ikalazimika kutuma walinda amani bila kupewa idhini na taifa mwenyeji,
muungano huo utatumia kwa mara ya kwanza kifungu kwenye mkataba wake, kinachouruhusu
kuingilia kati katika mataifa mengine nyakati za hatari kubwa.
Baadhi
ya mambo ambayo muungano huo unaruhusiwa kuingilia kati kuzuia ni uhalifu wa
kivita, mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.
Maafisa
wa UN wameonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na hatari ya kutumbukia kwenye vita
vya wenyewe kwa wenyewe.
Mauaji
mabaya zaidi yalitokea Ijumaa wiki iliyopita wapiganaji waliposhambulia maeneo
ya jeshi Bujumbura.
Jeshi
lilisema watu 87 waliuawa.
AU
hata hivyo bado itahitaji kupewa idhini na Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kuingilia kati.
source BBC
Post a Comment